Sunday, January 31, 2016

HII HAPA TAARIFA YA SERIKALI YA ERITREA KUTOA AMRI KWA WANAUME KUOA WAKE WAWILI...SASA UNAAMBIWA MAPYA YAIBUKA>>




Habari ya mzaha kwamba wanaume wa taifa la Eritrea wameagizwa kuoa wake wawili, ambayo imesambaa barani Afrika imewaudhi maafisa wa taifa hilo.

''Hata mwendawazimu katika mji mkuu wa Asmara atajua kwamba habari hii sio ya kweli'',afisa mmoja wa ubalozi wa Eritrea Kenya ameiambia BBC.

Habari hiyo ilichapishwa katika mtandao wa kitengo cha gazeti la The Standard la Kenya cha Crazy Monday.

Baadhi ya watu wametoa maoni yao katika mtandao wa Twitter kwamba wako tayari kusafiri hadi Eritrea ili kutafuta wanawake wa kuoa.

''Jarida la Crazy Monday ambalo huchapishwa na gazeti la Standard hujulikana sana kwa stori zake za udaku, likiwa ni mpango wa kutaka kuwavutia vijana," anasema Mathias Muindi wa BBC Media Monitoring.

Lakini hilo halijazuia taarifa hiyo kuripotiwa katika mataifa ya Nigeria hadi Afrika Kusini huku wengine wakisema kuwa ni ukweli.

Habari hiyo inasema kwamba ili kuhakikisha kuwa kuna wanaume walio wachache nchini humo wanaokidhi mahitaji ya wanawake walio wengi, kufuatia vita kati ya taifa hilo na Ethiopia mwaka 1998-2000, kila mwanamume lazima aowe wake wawili la sivyo afungwe jela.
Lakini afisa wa ubalozi wa Eritrea aliyezungumza na BBC amesema idadi ya wanawake na wanaume inakaribiana.

Waziri wa habari nchini Eritrea Yemane Gebremeskel alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter akisema kwamba habari hiyo ni ya uvumi, sio ya kweli na inakera.

0 Responses to “HII HAPA TAARIFA YA SERIKALI YA ERITREA KUTOA AMRI KWA WANAUME KUOA WAKE WAWILI...SASA UNAAMBIWA MAPYA YAIBUKA>> ”

Post a Comment

More to Read