Saturday, June 20, 2015
NEYMAR KWAHERI COPA AMERICA, APIGWA PINI MECHI NNE NA FAINI YA KUTOSHA
Do you like this story?
Nyota wa Brazil
na klabu ya Barcelona Neymar hatocheza tena michuano ya Copa America
inayoendelea huko Chile baada ya kufungiwa kucheza mechi nne kutokana na
kitendo chake cha utovu wa nidhamu alichokifanya wakati Brazi ikicheza dhidi ya
Colombia mchezo ambao ulimalizika kwa Brazil kufungwa kwa goli 1-0.
Nahodha huyo wa
Brazil alioneshwa kadi nyekundu baada ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi kupulizwa
kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Santiago Jumatano iliyopita. Neymar
alimpiga na mpira mgongoni kwa makusudi mchezaji Pablo Armero wa Colombia mara
baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya mwisho kumaliza mchezo huo.
Awali
alifungiwa kucheza mechi moja, lakini baadae shirikisho la soka la Amerika ya
Kusini (South America Football Confederation) liliongeza kifungo na faini ya
dola 10,000 za Kimarekani baada ya Neymar kugundulika kuwa alimtolea maneno
machafu mwamuzi Enrique Osses raia wa Chile. Kwahiyo sasa adhabu ya Neymar ni
kifungo cha kutocheza mechi nne pamoja na faini ya dola 10,000 za kimarekani
Naye Carlos
Bacca wa Colombia amefungiwa kucheza mechi mbili na faini ya dola 5,000 za
kimarekani baada ya kuhusika kwenye vurugu zilizotokea kwenye mchezo huo ambapo
yeye alimsukuma Neymar mara baada ya kumpiga Armero kwa mpira.
Lakini
shirikisho hilo la mpira la America ya Kusini limesema, rufaa ikowazi wa wote
waliopewa adhabu na Brazil wanaweza kupinga maamuzi hayo yaliyotolewa kabla ya
mchezo wao wa mwisho wa kundi C dhidi ya Venezuela utakaopigwa leo (Jumamosi)
usiku kuamkia kesho (Jumapili).
Kwasasa Brazil
wanaoongoza kundi C na wanakutana na Venezuela ambao wametoka kupoteza mchezo
wao dhidi ya Peru lakini wakiwa wameshinda mechi yao ya ufunguzi dhidi ya
Colombia.
Awali Neymar
alianza kuonesha vitendo ambavyo si vya kiungwana kwenye soka pale alipojaribu
kufunga goli kwa kutumia mkono lakini baadae ‘akambabua’ na mpira Pablo Armero
na kutaka kumpiga kichwa Jeison Murillo.
Kukosekana kwa
Neymar kutamfanya kocha wa Brazil Carlos Dunga amtumie Robinho kama mbadala wa
Neymar kwenye mechi ijayo dhidi ya Venezuela.
Dunga amekuwa
akiwatumia Robinho na Douglas Costa kwenye mazoezi ili kujaribu kutengeneza
uwiano mzuri kati yao wakati pia kiungo wa Liverpool Philipe Coutinho
anatarajiwa kuanza kwenye mchezo huo ambao utakuwa ni wa kwanza kwake tangu
kuanza kwa mashindano.
Robinho
amejumuishwa kwenye kikosi cha Dunga mwaka jana baada ya kuikosa michuano ya
kombe la dunia wakati huo kocha akiwa Scolari. Robinho ambaye alishawahi
kukipiga Real Madrid, Manchester City na AC Milan kwasasa anacheza kwenye klabu
ya Santos ya Brazil.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NEYMAR KWAHERI COPA AMERICA, APIGWA PINI MECHI NNE NA FAINI YA KUTOSHA”
Post a Comment