Monday, September 8, 2014

WATANZANIA 7 WAMEUAWA KWA RISASI NCHINI ZAMBIA NA WATU WASIOJULIKANA.


Polisi wa Zambia wakibeba Miili ya watanzania

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi



MIILI ya watu saba inayosadikiwa kuwa ni raia wa Tanzania, imekutwa imeuawa katika Kijiji cha Chianga kilichopo Wilaya ya Nakonde Nchini Zambia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Zambia, zinaeleza kwamba polisi kutokanchini humo walipata taarifa kutoka kwa wananchi ambapo walifika na kuikuta miili ya watu hao saba ikiwa imepoteza maisha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amesema kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka nchini Zambia, zimeeleza kwamba  tukio hilo limetokea Septemba 5, mwaka huu katika kijiji cha Chianga Wilayani Nakonde nchini Zambia.

Amesema, kwa mujibu wa maelezo kutoka nchini humo, yameeleza kwamba mara baada ya kuikuta miili hiyo walifanya uchunguzi wa awali na kubaini kuwa miili hiyo ilikuwa na majeraha ambayo hayakuweka bayana kwamba yametokana na nini.

Amesema, pia maelezo hayo yalithibitisha kwamba raia hao si wa nchini Zambia na kwamba  miili hiyo ilipokaguliwa mmoja alikutwa na kifaa cha kutunzia funguo kikiwa kimeandikwa KATAVI, mwingine alikutwa na picha zikiwa na nembo ya muhuri wa studio  iliyopo eneo la Kabwe Jijini Mbeya, huku wengine wakiwa wamevaa mask usoni.

Aidha, askari hao wakutoka nchini Zambia walisafirisha miili hiyo mpaka nchini Tanzania na kuikabidhi kwa askari  polisi watanzania waliopo katika kituo cha Tunduma kilichopo Wilayani Momba Mkoani Mbeya.

Aidha, Kamanada Msangi, amesema kuwa miili ya marehemu hao  saba imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya  Mbeya.

Hata hivyo, Msangi, aliwataka wananchi kufika katika hospitali ya Rufaa Mkoani hapa  kwa ajili ya utambuzi na kwamba askari wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini vifo vya watu hao vimetokana  nini.

0 Responses to “WATANZANIA 7 WAMEUAWA KWA RISASI NCHINI ZAMBIA NA WATU WASIOJULIKANA.”

Post a Comment

More to Read