Monday, September 8, 2014
TAARIFA ZINAZOZAGAA KUWA BABU SEYA NA MWANAE WAMEACHIWA HURU NI UZUSHI MTUPU,SOMA TAARIFA HII KUTOKA JESHI LA MAGEREZA
Do you like this story?
Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na
mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili
wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani. Wafungwa hao wanaotajwa ni Nguza
Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa jina la Papii
Kocha).
Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote
zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga
kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea kutumikia
adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.
Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu
huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza
ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa
kisheria.
Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini
wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la
kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.
Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM.
Septemba 8, 2014.Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi
wa simu (SMS) na mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa
wawili wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani. Wafungwa hao wanaotajwa ni
Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa jina la
Papii Kocha).
Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote
zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga
kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea kutumikia
adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.
Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu
huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza
ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa
kisheria.
Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini
wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la
kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.
Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM.
Septemba 8, 2014.
Source:othmanmichuzi.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAARIFA ZINAZOZAGAA KUWA BABU SEYA NA MWANAE WAMEACHIWA HURU NI UZUSHI MTUPU,SOMA TAARIFA HII KUTOKA JESHI LA MAGEREZA”
Post a Comment