Sunday, January 31, 2016

DRC KUCHUNGUZA DAFTARI LA WAPIGA KURA


C


Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza kuwa italipia tena daftari la wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu ujao nchini humo.

Hatua ya kulipitia tena daftari la wapiga kura inakuja katika hali ambayo hadi sasa bado hakuna maadalizi ya maana kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Mwishoni mwa kikao cha wawekezaji wa kigeni na Tume ya Huru ya Uchaguzi ya Kongo (Céni), Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Évariste Boshab amesema kuwa, serikali imeazimia kudhamini fedha kwa ajili ya marekebisho ya daftari hilo.(VICTOR)

Kwa upande wake, Corneille Nangaa, mkuu wa tume hiyo ya uchaguzi amesema shughuli ya marekebisho hayo itaanza tarehe 10 mwezi ujao wa Februari.

Hivi karibuni mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliitaka Tume ya Uchaguzi nchini humo kuorodhesha vijana waliotimiza umri wa miaka 18 katika daftari la kudumu la wapiga kura sanjari na kulifanyia marekebisho daftari hilo.

Kwa miezi kadhaa sasa, jamii ya kimataifa imekuwa ikisisitizia umuhimu wa kufanyika uchaguzi mkuu katika tarehe iliyopangwa huko Congo DR, huku waungaji mkono wa Rais Joseph Kabila wakitaka muda zaidi kwa ajili ya shughuli hiyo. Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, Rais Joseph Kabila haruhusiwi kugombea tena katika uchaguzi ujao.CHANZO:IRIB SWAHILI

0 Responses to “ DRC KUCHUNGUZA DAFTARI LA WAPIGA KURA”

Post a Comment

More to Read