Friday, June 6, 2014

JOSE MOURINHO AVUTIWA NA FABREGAS, PIQUE ASEMA `DILI` LIMEKAMILIKA KWA PAUNDI MILIONI 26.8


Amekiri:Bosi wa Chelsea. Jose Mourinho amesema klabu yake inavutiwa kumsajili nyota wa zamani wa Asernal.

Dili limekamilika: Cesc Fabreagas amehamia Chelsea, kwa mujibu wa mchezaji mwenzake wa Hispania Gerard Pique.

Mchezaji mwenzake? Fabregas anaweza kujiunga na mshambuliaji wa Hispania Diego Costa katika dimba la  Stamford Bridge msimu ujao.

KOCHA `mbwatukaji` Jose Mourinho amekiri kuwa Chelsea inavutiwa kumsajili Cesc Fabregas kutoka klabu ya FC Barcelona, huku mchezaji mwenzake wa Hispania Gerard Pique amesema dili hilo limekamilika kwa paundi milioni 26.8.

Kocha huyo amesema kuwa ni wazi Fabregas anataka kurudi ligi kuu ikiwa ni miaka mitatu imepita tangu aondoke Asernal, hivyo anafuatilia kwa makini ili kumsajili baada ya kombe la dunia.
Wakati huo huo Chelsea wako tayari kumpa ofa ya mshahara wa paundi milioni laki mbili kwa wiki winga wao hatari,  Eden Hazard ili kuwaziba mdomo Paris Saint-Germain wanaoiwinda saini yake.

Juu ya kiungo wa Hispania, Mourinho alisema: "Kwa kiasi fulani tunavutiwa na Fabregas. Ninafuatilia hali halisi. Inaonekana yuko tayari kuondoka Barcelona na anavutiwa kurudi England. Hili liko wazi. Lakini sio leo wala kesho au kabla ya kombe la dunia".

"Kuna mchakato huko anakotaka kuondoka, anataka kuja England kwasababu ni taifa analopenda kucheza. Tunavutiwa kufuatilia hali halisi".

Wakati huo huo, Pique kwa upande wake anasema dili hilo limekalimika. Beki huyo wa Hispania alinaswa na Kamera mjini Washington akimwambia kocha wa Hispania , Vicente del Bosque kuwa  Fabregas ataondoka Barcelona kwa dau la paundi milioni 26.8 baada ya klabu hiyo kumalizia msimu bila kikombe.

0 Responses to “JOSE MOURINHO AVUTIWA NA FABREGAS, PIQUE ASEMA `DILI` LIMEKAMILIKA KWA PAUNDI MILIONI 26.8”

Post a Comment

More to Read