Friday, June 6, 2014
PESA NDEFU YATUMIKA KATIKA KUTENGENEZA VIDEO MPYA YA DIAMOND NA IYANYA,LONDON,DAVIDO NDANI
Do you like this story?
Wiki
iliyopita Diamond Platnumz alikua London Uingereza kwa ajili ya kufanya show
lakini pia vilevile kufanya video ya wimbo wake aliofanya na msanii Iyanya wa
Nigeria.
meneja Babtale ambae anasimamia kazi za Diamond sasa hivi ambapo
amesema kutokana na kupiga hatua kwa Diamond na kuingia kwenye levo za
kimataifa, imebidi waanze kufanya video za kiwango hicho cha kimataifa lakini
haimaanishi kwamba ndio Platnumz hatofanya tena video Tanzania’
Namkariri
Tale akisema ‘video tuliyofanya na Iyanya Uingereza ni kwa sababu tulikua
tunamuhitaji Director MoE Musa ambae anaishi na kufanya kazi zake Uingereza
ndio maana tukasafiri mpaka huko, kuna video ambayo tutafanya Nigeria
tukishatoka Ghana na pia ikitokea kwamba tunatakiwa kufanya video Tanzania
tutafanya hivyo’
Bab Tale: ‘kiukweli tunaumia,
tunaumia kwa sababu kumlipa Moe Musa na kupata kila kitu kama kwenye hii video
ya juzi tumemlipa Moe peke yake dola elfu 25 ambazo zinagonga mpaka milioni 40
za Kitanzania, bado usisahau tumewatoa kina Iyanya Nigeria kwa hela yetu
kuwaleta London, kuwalipia nauli ya business class kwenye ndege na hoteli
hawawezi kulala hoteli mbaya kama sisi watoto wa Manzese’
Kwenye
sentensi nyingine, Babtale ameithibitishia kwamba Diamond atasikika tena kwenye
kolabo nyingine na Davido itakayowahusisha pia Tiwa Savage wa Nigeria na
Mafikizolo wa South Africa ikiwa ni kampeni ya kituo kimoja kikubwa cha TV
Afrika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “PESA NDEFU YATUMIKA KATIKA KUTENGENEZA VIDEO MPYA YA DIAMOND NA IYANYA,LONDON,DAVIDO NDANI”
Post a Comment