Friday, June 6, 2014
WASIO NA MAKAO WAANDAMANA BRAZIL.
Do you like this story?
![]() |
Maelfu waandamana kupinga kombe la dunia |
![]() |
10,000 Waandamana kupinga Kombe la Dunia |
Maelfu ya wenyeji wasio na makao mjini Sao Paolo waliandamana nje ya
uwanja utakaoandaa mechi ya kwanza ya kombe la dunia alhamisi ijayo wakipinga
gharama ya juu ya mashindano hayo.
Maandamano
hayo yaliwadia siku moja tu baada ya rais wa Brazil Dilma Rousseff
kuwahakikishia wageni na mashabiki wa kandanda kuwa kamwe hatoruhusu maandamano
yatie doa kwenye kipute hicho cha kombe la dunia.
Takriban
waandamanaji 10,000 waliziba barabara zote mjini Sao Paolo wakiishinikiza
serikali ya bi Rousseff iwekeze katika sekta ya afya elimu na ipunguze gharama
ya juu ya usafiri wa umma.
Zaidi
ya watu milioni moja waliandamana katika barabara za miji yote ya Brazil
wakishinikiza serikali kupunguza ubadhirifu wa fedha na kupunguza matumizi yake
kwa maandalizi ya kombe la dunia na yale ya Olimpiki yatakayofanyika mjini Rio mwaka
wa 2016.
Licha
ya hakikisho la rais Rousseff wafanyikazi wa reli walitishia kuanza mgomo upya
huku polisi wa trafiki mjini Sao Paolo pia wakitishia kuanza mgomo Alhamisi.
Mapema
wiki hii serikali iliwaongezea polisi wote mshahara ilikuzuia mgomo uliotishia
kuporomosha hali ya utengamano huku fainali ya kombe la dunia likinukia.
Serikali
imeahidi kutumia polisi na hata jeshi la taifa kudumisha amani na utengamano
wakati wa kombe la dunia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WASIO NA MAKAO WAANDAMANA BRAZIL.”
Post a Comment