Friday, June 6, 2014
KIJANA ALIYEDAIWA KUPOTEA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA MKOANI MARA APATIKANA AKIWA KATIKA HALI YA KUTISHA
Do you like this story?
Kijana mmoja mkazi wa kijiji cha Nyambogo wilayani Rorya mkoani Mara, ambaye anadaiwa kupotea nyumbani kwa imani za kishirikina hatimaye amepatikana huku akiwa katika hali ya kutisha bila kujitambua na mwili wake ukiwa umejaa tope jingi, tukio ambalo limevuta mamia ya wananchi wa kijiji hicho.
Kijana huyo Kenedy oguko mwenye umri wa
miaka 22 amekutwa nje ya nyumba yao asubuhi ya Juni 5 mwaka huu akiwa uchi wa
mnyama,ambapo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa tangu
kutoweka kwa kijana huyo siku nne zilizopita,wamekuwa wakimtafuta bila
mafanikio huku wakihusisha tukio hilo na imani za kishirikina.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM
wilaya ya Rorya Bw Samwel Kiboye,ambaye ni miongoni mwa mashuhuda wa
tukio hilo amewaomba wananchi kuacha kulipiza visasi kwa kuwasaka watu
wanaotuhumiwa kwa ushirikina bali watumie vyombo vya dola huku mwenyekiti wa
kijiji hicho akilaani vikali vitendo hivyo vya ushirikina vinavyoendelea
kijijini hapo hatua ambayo amesema imesabisha wananchi sasa kuishi kwa hofu
kubwa.
Hata hivyo katika hali ya kushangaza
wazee wa jadi kijijini hapo waliagiza kila mwananchi kupita mbele ya kijana
huyo na kumpa mkono kama njia moja wapo ya kuwezesha kupata fahamu kitendo
ambacho hata hivyo hakikuzaa matunda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)





0 Responses to “KIJANA ALIYEDAIWA KUPOTEA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA MKOANI MARA APATIKANA AKIWA KATIKA HALI YA KUTISHA ”
Post a Comment