Saturday, June 7, 2014
MAWAZIRI WAAHIDI MAMBO MAKUBWA.
Do you like this story?
Baada
ya Mawaziri na Manaibu Waziri kuapishwa jana na Rais Jakaya Kikwete, wametoa
ahadi lukuki kwa Watanzania kuhusu utendaji wao.
Mawaziri
saba na manaibu mawaziri 11 walikula kiapo mbele ya Rais Kikwete, huku wengine
watatu ikielezwa kuwa wataapishwa siku nyingine kutokana na kutokuwapo nchini.
Mabadiliko
ya Baraza la Mawaziri yalifanyika juzi ambapo mawaziri watano walitupwa na
kuingizwa 10 wapya, kupandishwa manaibu wanne kuwa mawaziri kamili na
kuwahamisha wengine wanane kutoka wizara zao kwenda nyingine.
Naibu
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema atafanya kazi kwa jitihada kubwa,
uadilifu, ushirikiano na kutoa huduma kwa wakati.
Nchemba
ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM amesema, “Nitafanya kazi kwa jitihada za
hali ya juu, uadilifu, ushirikiano na kutoa huduma kwa wakati. Watu wanadhani
kuingia Wizara ya Fedha ni kuchota fedha, binafsi nakwenda kusimamia sera”
Amesema
moja ya mambo atakayohakikisha kuwa anamshauri Rais Kikwete ni pamoja na
kuhakikisha kuwa nchi inaachana na utaratibu wa kuwa na bajeti tegemezi.
“Kuongeza
vyanzo vya mapato kutakuja kama ukusanyaji wa kodi unasimamiwa ipasavyo na
kupunguza matumizi ya Serikali,” alisema.
Alisema
jambo jingine atakalolifanya ni kumshauri Rais kuhusu Sheria ya Ununuzi lengo
likiwa ni kuondokana na ununuzi wa vitu mbalimbali kwa mtindo wa zabuni, kwa
maelezo kuwa mtindo huo huifanya Serikali kutumia kiasi kikubwa cha fedha.
“Jambo
hili la ununuzi ni pana na linahitaji kushauriana na kufanya uchambuzi wa
kitaalamu. Pia nitashirikiana na wenzangu kuhusu kuminya mianya mingine
inayochangia Serikali kukosa mapato yake ikiwa ni pamoja na kushirikiana na
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),” alisema Nchemba.
Kwa
upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria, Asha Rose Migiro alisema moja ya
majukumu atakayoyafanya ni kuhakikisha kuwa mchakato wa Katiba Mpya unakwenda
kama ulivyopangwa, huku akisisitiza kuwa hawezi kukipendelea CCM katika
mchakato huo.
“Nitasimamia
mchakato wa Katiba katika kipindi hiki ambacho tunaelekea kwenye Bunge la
Katiba na baadaye Kura ya Maoni.
Jambo zuri ni kwamba mchakato huu unakwenda
kwa mujibu wa sheria. Nawahakikishia Watanzania nitafanya kazi kwa uaminifu na
kujituma,” alisema Migiro.
Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufunzi, Jenister Mhagama alisema sekta ya elimu
kwa muda mrefu imekuwa na changamoto nyingi na kwamba moja ya mambo
atakayoyafanya ni kuhakikisha kuwa anapambana na changamoto hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAWAZIRI WAAHIDI MAMBO MAKUBWA.”
Post a Comment