Saturday, June 7, 2014
MWEGANE YEYA AAHIDI MAKUBWA TAIFA STARS, AMSHUKURU MUNGU KWA KUITWA NA MART NOOIJ
Do you like this story?
MSHAMBULIAJI
hatari wa Mbeya City fc, Mwegane Yeya amefurahishwa na kitendo cha kuitwa
katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha
Mholanzi, Mart Nooij.
Akizungumza na
mtandao huu, Mwegane amesema kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kupata nafasi hiyo
kwasababu Tanzania ina wachezaji wengi wenye viwango vya hali ya juu, lakini
amechaguliwa yeye.
“Hii ni nafasi
nyingine muhimu kwangu. Niliwahi kuitwa katika kikosi cha Young Future Taifa
Stars na Kim Poulsen, lakini sikufanya vizuri kwasababu nilikuwa majeruhi.
Naamini kwasasa nitaitumia vizuri nafasi hii”. Alisema Mwegane ambaye ni hatari
kwa kufunga magoli ya kichwa.
Mwegane
aliongeza kuwa kuitwa na Nooij ni ishara ya kukubali kazi yake, hivyo anajiona
mwenye wajibu mkubwa wa kuisadia Stars kuelekea mchezo muhimu dhidi ya
Msumbiji.
Nyota huyu wa
Wagonga Nyundo wa Mbeya ni miongoni wa wachezaji wa Kikosi cha Taifa Stars
kinachotarajia kuingia tena kambini Jumatano (Juni 11 mwaka huu) ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya mechi ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya
Msumbiji itakayochezwa Julai 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa
Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Boniface Wambura Mgoyo, Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na kambi ya siku tatu
jijini Dar es Salaam ikijumuisha wachezaji 28. Kwa mujibu wa programu ya Kocha
Mart Nooij, Stars itaingia tena kambini Juni 24 mwaka huu.
Wachezaji
wanaotakiwa kuripoti kambini ni Deogratias Munishi, Aishi Manula, Benedictor
Tinoko, Kelvin Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub, Joram Nason, Shomari
Kapombe, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris na Pato Ngonyani.
Wengine ni
Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Said
Juma, Haruna Chanongo, Himid Mao, Said Ndemla, John Bocco, Simon Msuva, Kelvin
Friday, Ramadhan Singano, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Mwegane Yeya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWEGANE YEYA AAHIDI MAKUBWA TAIFA STARS, AMSHUKURU MUNGU KWA KUITWA NA MART NOOIJ”
Post a Comment