Monday, June 9, 2014

MGONJWA AFIA WODINI WAKATI DAKTARI AKIPIGANA NGUMI NA MWENYE MGONJWA MOROGORO


Mwili wa marehemu Yasin Jailan (15) aliyekata roho ndani ya wodi namba tisa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro huku dokta akizichapa kavukavu.

Baba wa marehemu (kushoto) akilia kwa uchungu.

Baadhi wanachi waliojaa hospitalini kushuhudia mkasa huo.



Timbwili! Katika hali ya kusikitisha mgonjwa Yasin Jailan (15) aliyekuwa wodini anadaiwa kkata roho huku dokta akizichapa kavukavu na wagonjwa .

Akiwa mitaani akisaka matukio, mwanahabari wetu alivutiwa waya na chanzo chetu kisha akatonywa kuwa kuna bonge la timbwili kwenye wodi namba tisa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro ambapo alitii wito na kufika eneo la tukio ndani ya dakika sifuri (huwa Global hatulazi damu kufika eneo la tukio).

Alipofika wodini hapo, mwandishi wetu alishuhudia mtoto akikata roho huku baba mwenye mgonjwa aliyetajwa kwa jina la Jailan Mrisho akizichapa na daktari ambaye jina halikupatikana.

Baada ya kuona hali tete huku watu wakiwa na hasira wakimlalamikia daktari huyo kwa uzembe, mwanahabari wetu alipiga simu kituo kikuu cha polisi mkoani hapa ambapo polisi wa pikipiki almaarufu kama tigo walifika na kumchukua daktari huyo kisha kumkimbiza kituoni kumnusuru na kipiga kutoka kwa watu wengine ambao walifika hospitalini hapo kuwaona wagonjwa wao.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa, John Laswai alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi baada ya kumnusuru dokta huyo ambaye kwa sasa anadunda mtaani.

0 Responses to “MGONJWA AFIA WODINI WAKATI DAKTARI AKIPIGANA NGUMI NA MWENYE MGONJWA MOROGORO ”

Post a Comment

More to Read