Sunday, June 15, 2014
MJAMZITO AJIFUNGUA MJUSI BADALA YA MTOTO.
Do you like this story?
Mwanamke
mmoja nchini Indonesia amejifungua mjusi badala ya mtoto.
Mwanamke
huyo Debi Nubatonis, mwenye umri wa miaka 31, ameanza kupata vitisho kutoka kwa
kundi la vijana kutokana na kitendo hicho wakimtuhumu kwa uchawi ambapo sasa
mamlaka za nchi hiyo zimetuma timu ya wataalamu kwa ajili ya kumaliza utata wa
tukio hilo lisilo la kawaida.
Wanasayansi
katika timu inayofanya uchunguzi kwa mwanamke huyo wamesema wanahitaji kupatiwa
muda wa kutosha kuchunguza tukio hilo na kuja na maelezo ya kueleweka.
Kitendo
hicho cha mwanamke kujifungua mjusi badala ya mtoto kilibainishwa na mkunga
anayedai kwenda nyumbani kwa mwanamama huyo kumsaidia kujifungua katika kijiji
cha Oenunto kwakuwa alishindwa kufika hospitalini.
Madai
ya mwanamke huyo kujifungua mjusi yameibua vitisho dhidi ya mwanamke huyo na
familia yake ambao wanatuhumiwa kwa uchawi na kuamsha mjadala mkubwa katika
mitandao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MJAMZITO AJIFUNGUA MJUSI BADALA YA MTOTO.”
Post a Comment