Wednesday, June 18, 2014

RATIBA LIGI KUU ENGLAND YAANIKWA HADHARANI, VAN GAAL AKWEPA VIGINGI, MAN CITY YAANZA NA VISIKI


Tutacheza na nani? Kocha wa Uholanzi,  Louis van Gaal ataanza kazi Manchester United baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la dunia.



LOUIS van Gaal amepewa mwanzo wa maisha mapya katika klabu ya Manchester United baada ya ratiba ya msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England kuwekwa hadharani.

 Hata hivyo Van Gaal amepewa mwanzo rahisi tofauti na kocha aliyemrithi, David Moyes aliyepewa mwanzo mgumu alipobeba mikoba ya Sir Alex Ferguson.
 
Kocha huyo anayeifundisha Uholanzi, baada ya fainali za kombe la dunia atajiunga Old Trafford na katika ratiba iliyotoka amepangwa kukutana na timu ya Swansea agosti 16 mwaka huu.

MECHI ZA UFUNGUZI

Arsenal v Crystal Palace

Burnley v Chelsea

Leicester City v Everton

Liverpool v Southampton

Manchester United v Swansea City

Newcastle United v Manchester City

Queens Park Rangers v Hull City

Stoke City v Aston Villa

West Bromwich Albion v Sunderland

West Ham United v Tottenham Hotspur
Mechi hizi zitachezwa Agosti 16/17

Baada ya mechi ya ufunguzi ya Man United zitafuatia mechi mbili za ugenini dhidi ya Sunderland na Burnley kabla ya kurudi nyumbani kukabiliana na Queens Park Rangers septemba 13.

Kiukweli, United hawatakutana na wapinzani wao wa ubingwa mpaka mwishoni mwa mwezi Agosti watakapoikaribisha Chelsea ya Jose Mourinho.
Hii itakuwa nafasi nzuri kwa Van Gaal kuutumia vyema uwanja wa mazoezi wa Carrington wakati huu klabu ikihitaji kufuta majanga ya David Moyes msimu uliopita.

Kwa upande wa mabingwa, Manchester City watakabiliana na upinzani mkubwa baada ya kupanga kukutana na  Liverpool, Arsenal  na Chelsea katika mechi za ufunguzi.Kikosi cha Manuel Pellegrini kitawakaribisha wekundu wa Anfield agosti 23 kabla ya kuwakaribisha Chelsea uwanja wa Etihad septemba 20.

MECHI ZA UNITED

Mar 14: Spurs (H)
Mar 21: L'pool (A)
Apr 4: Villa (H)
Apr 11: City (H)
Apr 18: Chelsea (A)
Apr 25: Everton (A)

0 Responses to “RATIBA LIGI KUU ENGLAND YAANIKWA HADHARANI, VAN GAAL AKWEPA VIGINGI, MAN CITY YAANZA NA VISIKI”

Post a Comment

More to Read