Wednesday, June 18, 2014
TANZANIA YABADILI SHERIA KUHUSU SHISHA
Do you like this story?
Waziri
wa afya nchini Tanzania, amesema kuwa Tanzania inapanga kutathmini sheria ya
sasa kuhusu matumizi ya Sisha ili kufanya mageuzi au kubadili sheria hiyo
matumizi ya Shisha.
Dkt
Seif Rashid Selemani amesema kuwa sheria hiyo italenga kulinda afya ya
watanzania hasa walio na uraibu wa Shisha na pia kuhakikisha kuwa wanaotumia
Shisha katika sehemu zengine duniani wanapata kubadili mfumo wa maisha ili
kulinda afya zao.
Hii
ni baada ya taarifa ya awali kuwa serikali ilikuwa tayari imechukua hatua
kupiga marufu bidhaa hiyo ambayo inaenziwa sana hasa na vijana.
Uraibu
huo unaohusisha uvutaji wa Tumbaku yenye ladha tofauti tofauti ambayo hutiwa
ndani ya chupa kubwa na kuvutwa kwa mirija, umeshika kasi sana Tanzania hasa
miongoni mwa vijana mjini Dar Es Salaam.
Baadhi
ya watu wanaiona Shisha kama isiyokuwa na madhara ya kiafya ikilinganishwa na
uvutaji wa Sigara.
Lakini
wataalamu wanaamini kuwa uvutaji wa Shisha kwa muda wa saa moja ni sawa na
kuvuta sigara miamoja.
Madaktari
walitoa onyo kuhusu uvutaji wa Shisha wakisema kuwa waraibu wanakabiliwa na
tisho la kuugua Saratani sawa na hatari inayowakabili wavutaji wa sigara
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TANZANIA YABADILI SHERIA KUHUSU SHISHA”
Post a Comment