Wednesday, June 18, 2014
WAKUU WA POLISI WATUTWA KAZI LAMU KENYA
Do you like this story?
Inspekta wa polisi Kenya, David Kimaiyo |
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta |
Idara
ya polisi nchini Kenya imefanya mabadiliko ya dharura katika afisi kuu za
Kaunti ya Lamu, kutokana na mashambulio yaliyosababisha vifo vya watu 60 wiki
hii.
Inspekta
mkuu wa polisi nchini Kenya David Kimaiyo amechapisha katika mtandao wa jamii
Twitter, maelezo ya wakuu wa polisi katika kaunti hiyo waliofutwa kazi mara
moja, wakiwemo makamanda wa polisi.
Afisa
mkuu wa kituo cha Polisi, OCS, pia amehamishwa kituo mara moja.
Hatua
hii tayari imepokewa kwa hisia tofauti huku wakenya wengi wakielezea
kutoridhishwa na adhabu hiyo.
Miongoni
mwa walioandika malalamiko yao kwa Bwana Kimaiyo, wamesema kuwa mabadiliko
yalistahili kufanyika hadi ngazi ya juu zaidi, baadhi hata wakimtaka yeye
mwenyewe kama Inspekta wa polisi kujiuzulu.
Tangu
kutokea shambulio la Jumapili usiku katika kijiji cha Mpeketoni, karibu na
kisiwa cha Lamu pwani ya Kenya, lawama zimeelekezwa kila upande, huku baadhi
wakidai kuwa wanasiasa wamehusika na wengine wakilalamikia utepetevu wa polisi
katika kutekeleza majukumu yao.
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta alihutubia taifa Jumanne akisisitiza kuwa ana imani
kuwa mashambulio hayo yalichochewa kisiasa.
Ametoa
matamshi hayo licha ya taarifa kutoka kwa kundi la wapiganaji wa kiislamu wa AL
shabaab waliodai kuwa wao ndio waliohusika.
Matamshi
ya rais Kenyatta yame kejeliwa na wanasiasa wa upinzani nchini humo waliodai
kuwa rais huyo hana ufahamu wa yale yanayoendelea nchini mwake.
Seneta
kutoka chama kikuu cha upinzani, Moses Wetangula amesema matamshi ya rais sio
ya kweli. '' Badala ya kuitisha usaidizi wa wenzetu wenye teknolojia bora, hata
tutumie ndege zisizo na rubani kuwalipua huko waliko, tunakaa hapa Nairobi na
kudai AL shabaab hawakuhusika.'' Wetangula aliambia bunge la Kenya. '' Huu ni
mzaha,'' Aliongeza bwana Wetangula.
Wakaazi
wengi wa Mpeketoni waliozungumza wametueleza kuwa, wanaamini shambulio la
Jumapili usiku linatokana na mzozo wa ardhi kati ya jamii zinazoishi huko.
Wakaazi
hao wamesema kuwa Al shabaab wamedakia tu kujigamba kwa yaliotokea huko ila wao
wanaamini kuwa ni jambo lililokuwa likitokota kwa muda mrefu.
Huku
hayo yakiarifiwa, polisi wanasemekana kuimarisha doria katika eneo la Lamu na
vitongoji vyake. Wanajeshi wachache wametumika kuimarisha usalama hasa katika
kijiji cha Mpeketoni.
Katika
taarifa zilizotufikia ni kuwa Polisi wameimarisha usalama katika mkoa wa
magharibi mwa Kenya kutokana na duru walizopokea kuwa huenda eneo hilo
likalengwa kwa shambulio.
Al
shabaab wamefanya mashambulio ya mara kwa mara katika sehemu mbali mbali nchini
Kenya tangu majeshi ya Kenya yaingie nchini Somalia mwaka wa 2011, katika
oparesheni ya kuwafagia kutoka nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAKUU WA POLISI WATUTWA KAZI LAMU KENYA”
Post a Comment