Thursday, June 12, 2014

SINA MPANGO WA KUMUUZA HAZARD - MOURINHO.



MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amepuuza tetesi zilizozunguka mustakabali wa Eden Hazard na kudai kuwa hawezi kumruhusu nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kuondoka katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

 Hazard mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda kwa mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain huku kocha wake Laurent Blanc akidai hadharani kwamba anamuhitaji mshambuliaji huyo.

 Pamoja na kutofurahishwa na kiwango cha Hazard wakati wa msimu uliopita wa Ligi Kuu, Mourinho sasa amethibitisha kuwa hana mpango wowote wa kumuachia nyota huyo wa zamani wa Lille.

 Mourinho amesema kwasababu alisema Hazard hana kila anachotakiwa kuwa nacho mshambuliaji hajamaanisha kwamba alikuwa hamuhitaji mchezaji huyo kwani bado ataendelea kuwepo katika mipango yake katika siku nyingi zijazo atakazokuwepo Chelsea. Hazard ni mfungaji anayeongoza kwa mabao kwenye timu hiyo msimu uliopita akiwa amefunga mabao 14 na kutoa usaidizi mara saba.

0 Responses to “SINA MPANGO WA KUMUUZA HAZARD - MOURINHO. ”

Post a Comment

More to Read