Thursday, June 12, 2014

MAZOEZI YA ARGENTINA YAVAMIWA NA RONALDINHO `FEKI`, MESSI APIGIWA MAGOTI NA KUFUTWA VIATU...HATARI!


Nakujua wewe! Shabiki anayeonekana kama Ronaldinho alivamia mazoezi ya Argentina kwenye uwanja wa Belo Horizonte

Nyota akigoma kutoka: Messi akifurahia wakati shabiki akitolewa na maofisa, kufafana na Ronaldinho kulimfanya Messi acheke sana

Messi aliamua kumkumbatia jamaa.

Shabiki akifuta kiatu cha kulia cha Lionel Messi baada ya kuvamia uwanjani wakati wa mazoezi

MAZOEZI ya Argentina jana jumatano yalivamiwa na mtu moja mwenye sura inayofahamika duniani.

Wakati Lionel Messi na wachezaji wenzake wakijiandaa kuelekea mchezo wa ufunguzi wa kundi lao dhidi ya Bosnia siku ya jumapili, shabiki mmoja mwenye sura inayofanana na nyota wa zamani wa Brazil, Ronaldinho alivamia uwanjani.

Waargentina walimfurahia jamaa huyo lakini alitolewa na maofisa wa uwanja.
Mashabiki wengi walivamia uwanjani na kumpigia magoti nahodha huyo wa Argentina, Lionel Messi huku wakifuta viatu vyake.

Messi alicheka tu na aliwakumbatia mashabiki hao na alimpa shabiki mmoja sweta lake kabla ya walinzi kumtoa. 

Mashabiki wengine waliukimbilia mpira ambao Muargentina huyo alikuwa anautumia katika mazoezi.

0 Responses to “MAZOEZI YA ARGENTINA YAVAMIWA NA RONALDINHO `FEKI`, MESSI APIGIWA MAGOTI NA KUFUTWA VIATU...HATARI!”

Post a Comment

More to Read