Thursday, June 12, 2014
KUMEKUCHA BRAZIL,DIMBA KU"NGOA NANGA
Do you like this story?
Kombe
la dunia Brazil 2014 linatarajiwa kungo'a nanga baadaye leo jioni huku Brazil
na Croatia wakitoana kijasho mjini Sao Paolo.
Dimba
hilo litakalodumu kwa mwezi mmoja, litashuhudia mataifa 32 yakimenyana kuwania
kombe hilo katika fainali itakayochezwa mjini Rio tarehe 13 Julai.
Mechi
ya ufunguzi itaanza baada ya sherehe ya kufungua mechi hiyo mjini Sao Paulo. Ni
mechi ambayo itakuwa inatoa kipaombele kuonyesha umuhimu wa kukuza vipaji, utu
na kabumbu.
"wacheni
niwambie kuwa wakati umewadia. Tunaenda sote . Hili ni kombe letu la dunia, ''
alinukuliwa akisema kocha wa Brazil Luis Felipe Scolari.
Mwaka
jana zaidi ya watu milioni moja walishiriki katika maandamano ya kupinga hatua
ya serikali kuandaa michezo hiyo kwa gharama ya juu wakati wananchi wengi
wakiishi kwa umasikini.
Serikali
ya Brazil iko makini kuzuia kutokea tena kwa ghasia zilizoshuhudiwa wakati wa
maandamano hayo. Rais Dilma Rousseff amesema kuwa hatakubali kamwe maandamano
yanayosababisha ghasia kuathiri kombe la dunia.
Maelfu
ya polisi na wanajeshi watashika doria nchini humo kuhakikisha kuwa mechi
zinafanyika bila vurufu.
England
itacheza mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Italy Jumamosi tarehe 14 , mechi ambayo
itapeperushwa moja kwa moja
Timu
hiyo pia itacheza dhidi ya Uruguay na Costa Rica katika kundi D.
Wenyeji
Brazil wataanza mechi leo wakipigiwa upatu kushinda kombe la dunia kwa mara ya
sita wakati mabingwa watetezi Hispania nao wanakilenga kushinda kombe hilo kwa
mara ya nne baada ya kushinda ubingwa wa Ulaya miaka miwili iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KUMEKUCHA BRAZIL,DIMBA KU"NGOA NANGA”
Post a Comment