Thursday, June 12, 2014

WATU 10 WATIWA MBARONI NA POLISI KUFUATIA VURUGU ZILIZOTOKEA JIJINI MWANZA



Polisi jijini Mwanza imelazimika kutumia mabomu ya machozi kufuatia vurugu za baaadhi ya wafanyabiashara wadogo maaarufu kama machinga na watoto wa mitaani wakipinga kupinga zoezi la kuhamishwa eneo la Makoroboi walilokuwa wakifanyia biashara hapo awali.

Zoezi hili limesababisha wafayabiashara mbalimbali kufunga biashara zao na wengine kupoteza mizigo kutokana na vurugu hizo huku idadi kubwa ya wananchi wakishindwa kuendelea na shuguli zao

Nia aina ya vurugu zilizo tokea kwa takribani masaa matano katikati ya jiji la Mwanza baada ya halmashauri ya jiji kulazimika kuvunja vibanda vya wafanya biashara wakidai kukaidi agizo la mpango wa kusafisha jiji.

Vurugu hizi zimelazimu wafanyabiashara wote jijini hapa kusitisha utoaji wa huduma za kibiashara kwa wananchi

Baadhi ya Wamachinga katika eneo la makoroboi waliungwa mkono na watoto wa mitaani jambo lilowapa wakati mgumu jeshi la polisi katika kuthibiti vurugu zilizodumu kwa muda

Ilikuwa ni vigumu kwa mwananchi kuingia na kutoka katikati ya jiji, wakihofia usalama wa maisha yao, waliokuwa maeneo ya vurugu walilazimika kufungiwa ndani ya soko na katika maeneo mengine ili kulinda usalama.

Mwenyekiti wa wamachinga mkoa wa Mwanza Joseph Mwita amekana kuhusika kwa wamachinga katika vurugu hizi na kuwahusisha vijana wasio na kazi kutumia mwanya huu kuleta vurugu ili kupora vitu mbalimbali kutoka kwa wafanya biashara na wananchi

Licha ya jeshi la polisi kufanikiwa kuthibiti vurugu hizi kwa kutumia nguvu ya ziada mkiwemo vilungu halmashauri yajiji la Mwanza imesisitiza kuwa zoezi hili ni endelevu.

Katika haatua nyingine kituo cha haki za binadamu kimelaani kitendo hiki cha jeshi la polisi kutumia nguvu kupita kiasi huku kikiitaka serikali kuwa na mpango madhubuti wa ajira kwa vijana.

0 Responses to “WATU 10 WATIWA MBARONI NA POLISI KUFUATIA VURUGU ZILIZOTOKEA JIJINI MWANZA ”

Post a Comment

More to Read