Thursday, June 5, 2014

STAMICO YATWAA MGODI WA KIWIRA.



Hatimaye mgodi wa makaa ya kiwira  uliopo  wilayani ileje  umerudishwa rasmi serikalini kutoka Tan Power  Resources(TPR)  na kukabidhiwa kwa shirika la madini  la taifa (stamico) kwa ajili ya kufufua na kuendeleza mdodi huo.

Akizungumza wkati wa kukabidhi  mdogi huo kwa stamico makamu mwenyekiti  wa stamico  Alexander muganda  alisema kurudishwa serikalini kwa mgodi huo kunatokana  na serikali na TPR kufikia  muafaka kwa  serikali kuuchukua mgodi kwa asilimia 100

Muganda alisema uendeshaji wa mgodi  chini ya stamico umegawanyika  katika sehemu  nne sehemu yakwanza  ni upanuzi wa mgodi chiniya aridhi ujenzi wa mgodi wa wazi katka eneo la ivogo ujenzi wa mitambo ya kufumua umeme  pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme.

Uendeshaji wa magodi huu pia utahusisha ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wenye uwezo kufua  megawati 200 za umeme na ujenzi  wa njia ya kilometa 100  kwa ajili ya kusafirisha.

Umeme wa kv 22 alisema  na kuongeza kuwa stamico imepanga kufanyia ukarabati mashine ya kufua umeme megawati sita.

Aidha alisema ukarabati huo unatarajia kugharimu sh bilioni 18.6  na kwamba utahusisha sehemu za  uzalishaji wa makaa mawe uzalishaji  umeme mtambo  wa kusafishia karakana sampuli na maabara mtaji unaohitjika kueneleza mgodi  huu ili kuzalisha megawati 200  ni takribani dola za marekani milioni 400  alisema muganda.

Kaimu mkurugenzi mtendaji wa stamico Edwin ngonyani alitaka menejiment  ya mgodi  wa kiwira kubadilika kwa kuachan ana ukuu na kuw watendaji ili waendesh emgodi huo kwa mafanikio na kufikia matarajio ya watanzania.

0 Responses to “STAMICO YATWAA MGODI WA KIWIRA.”

Post a Comment

More to Read