Thursday, June 5, 2014

MBUNGE ATAKA WABAKAJI WAPEWE ADHABU YA KIFO



Mbunge wa chama cha CUF moza abeid  saidy ameiomba serikali kuweka adhabu ya kifo kwa wabakaji ili liwe fundisho kwa wtu wenye tabia kama  hizo.

Alisema hayo katika  swli lake la nyongeza bungeni jijini hapa  jana baada ya kutoridhika na majibu aliyopewa kwenye swali lake la msingi.

Kwanini serikali isitoe fundisho  kw watu wengine wenye tabia hizo pia serikali haina mpango  wa kuongeza adhabu kwa wabakaji kwani adhabu ya sasa ya kifungo cha maika 30 jela inatosha.

Alisisitiza kuwa  anakubaliana na mbunge huyo kuwa ubakaji unaendela kukua kwa kasi lakini adhabu  za sasa zinatosha kutoa fundisho kwa wahusika liwahimiza wote wenye  tabia hiyo chafu waache mara moja.

Katika swali lake la msingi moza aliuliza je ni kwasababu gani hukumu ya makosa ya ubakaji hutolewa tofauti ambapo  wengine huhukumiwa kifungo cha maisha  wakti wengine hufungwa kifungo cha miaka 15-50?

Akijibu swali hilo la msingi  kairuki alisema kubaka ni kosa la jinai  ambalo linatendeka katika mazingira yaliyoelezwa  chini ya kifungu cha 130(1) na (2)  cha sheria ya kanuni  za adhabu sura ya 16.

Naibu waziri  alisema adhabu ya kosa la kubaka limetamkwa  wazi na sheria za kanuni za adhabu  chini ya kifungu  cha 131 adhabu ya kosa hili chini ya sheria  hii ni kifunhgo cha miaka 30  au kifungo cha maisha pamoja na kuchapwa viboko  na kulipa faini.

Aliems pamoja na dhabu inayotolewa  chini ya kfiungu cha 131(1)  kifungu cha 131(3) kinabainisha kwamba endapo muathirika  wa ubakaji ni mtoto  mweye umri wa chini ya miaka 10  adhabu ya mbakaji atakapopatikana na hatia ni kifungo cha maisha.

0 Responses to “MBUNGE ATAKA WABAKAJI WAPEWE ADHABU YA KIFO”

Post a Comment

More to Read