Thursday, June 5, 2014

KAMWAGA AKIMBIA OFISI ZA SIMBA.



Dar es salaam fukuto la uchaguzi linaloendelea ndani ya klabu  ya simba limemfanya  katibu mkuu  wa klabu hiyo Ezekiel kamwaga  kuiona ofisi yake chungu kama  shubiri.

Kamwaga hajaingia ofisini kwa muda wa wiki moja sasa . jumatano iliyopita kamwaga lijikuta katika wakati mgumu baada ya kuziiwa na kundi la wanachama wa simba la Taliban kuingia ofisinikwake kile walichodai kuwa wakati wa kutangazwa kwa jina la Michael wmbura kuwa lemeenguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi  wa kuwania urais wa simba katbu huyo alicheka.

Ilikuwa kama sinema  wanachama walipimzuia kuingia kupitia  getini kamwaga  akazunguka kwa mlango wa nyumba ambako kuna mgahawa wa wasomali akataka kuruka ukuta ili aingie ofisini  lakini likwama baada ya wanachama hao kumtoa mbio na kwenda kujisalimisha kituo cha polisi  msimbazi.

Kimsingi  hakuna kitu kibaya nilichofanya nawashangaa wanachama kunizuia kuingia  ofisini tukio lile limenidhalilisha sana naapa sitakanyaga tena ofisini alisema kamwaga.


0 Responses to “KAMWAGA AKIMBIA OFISI ZA SIMBA.”

Post a Comment

More to Read