Thursday, June 5, 2014

SERIKALI YAENDELEA KUMKANA MASELLE



sakata la tuhuma za balozi wa uingereza nchini  dianna Melrose limeendelea kuchukua  sura mpya  na sasa mzigo huo unamwelema naibu  waziri wa nishati na madini stepheni maselle baada ya serikali kudai kwamba ilikuwa ni kauli yake na si msimamo wa serikali .

Jana waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji dk marry nagu  alitoa kauli bungeni  kuwa kauli inayopaswa kufuatwa kuhusu uhusiano baina  ya Tanzania na balozi  huyo  ni ili iliyotolewa na ikulu na si ya maselle bungeni.

Nagu alitoa kauli hiyo kwa niaba ya waziri wan chi ofisi  ya waziri mkuu sera uratibu na bunge na amesema katika hali ya kawaida   serikali inakuwa na kauli moja licha ya kuwa na vitengo vingi .

Nagu alitoa kauli ya serikali baada ya mwongozo wa spika ulioombwa na mbunge wa kigoma kusini david kafulila  ambaye litaka ufafanuzi kuhusu kauli tata.

Tofauti na miongozi mingine mwongozo  huo ulitolewa majibu ya papohapo  kwa naibu spika kumsimamisha dk nagu  aliyekuwa amekalia kiti cha mratibu wa shughuli za bunge

0 Responses to “SERIKALI YAENDELEA KUMKANA MASELLE”

Post a Comment

More to Read