Thursday, June 5, 2014
POLISI WANAOTUMIA PIKIPIKI MAARUFU KAMA "TIGO" WASHUSHIWA TUHUMA BUNGENI
Do you like this story?
Waziri mkuu mh Mizengo Pinda amesema
atazungumza na waziri wa mambo ya ndani kumuagiza kuhusu kero ya askari
wanaotumia pikipiki maarufu kama "tigo" kuwabugudhi madereva pikipiki
ili wachukuliwe hatua
Waziri mkuu Pinda ameyasema hayo
bungeni katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo wakati akijibu swali la
Mbunge wa Korogwe vijijini Mh. Steven Ngonyani kuhusu kero ya polisi hao
Katika swali lake amesema polisi hao
wamekuwa wakiwakamata madereva bodaboda na kuwatukana pamoja na kuwatoza faini
kubwa wakati mwingine bila kuwapa risiti jambo linaloweza kusababisha ugomvi
usio na maana
Mh. Pinda amesema kwa kuwa mbunge huyo
analifahamu tatizo hilo, atalipeleka kwa waziri wa mambo ya ndani kulifanyia
kazi mara moja, ili polisi wa aina hiyo waweze kuchukuliwa hatua za kisheria
baada ya kubainika kuwa ni kweli wamefanya kosa hilo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)

0 Responses to “POLISI WANAOTUMIA PIKIPIKI MAARUFU KAMA "TIGO" WASHUSHIWA TUHUMA BUNGENI ”
Post a Comment