Thursday, June 5, 2014
MCHUNGAJI ALIYEFUNGWA MIAKA 30 JELA KWA UBAKAJI AFUTIWA HUKUMU, MAHAKAMA YAMUACHIA HURU
Do you like this story?
Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya,
imebatilisha hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 aliyokuwa
akiitumikia Mchungaji wa Kanisa la EAGT la Iwambi Jijini Mbeya, Daniel
Mwasumbi(57) aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya ubakaji na kumpa mimba mwanafunzi
wa Shule ya Sekondari Itende Neema Beni(19) jijini hapa.
Mchungaji Mwasumbi alihukumiwa kifungo
hicho, Januari 2 mwaka huu na mahakama ya Wilaya ya Mbeya na Hakimu Gilbert
Ndeuruo na Serikali kuwakilishwa na wakili Achiles Mulisa, ambapo Mahakama
ilimtia hatiani Mchungaji katika makosa kinyume cha sheria kifungu cha 130(2)e
na 131(1) sura ya 16 ya sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Awali Mchungaji Mwasumbi alikuwa
akitetewa na Wakili wa kujitegemea Victor Mkumbe ambapo ilidaiwa kutenda makosa
hayo kati ya Januari 2008 hadi 2011 ambapo alimpa ujauzito na kumzalisha
mwanafunzi huyo watoto wawili wa kiume kwa nyakati tofauti hivyo kumkatisha
masomo kinyume cha sheria.
Katika Rufaa hiyo Mchungaji
Mwasumbi alikuwa akitetewa na Wakili wakujitegemea Benjamin Mwakagamba kutoka
Dar es Salaam wakati Serikali iliwakilishwa na Wakili Prosister Paul.
Akisoma hukumu ya rufaa hiyo, Jaji wa
Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Atuganile Ngwala, alisema kuwa sababu
zilizowasilishwa kwenye mahakama hiyo na Wakili wa upande wa utetezi
zilidhihirisha kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa kisheria kwenye hukumu hiyo.
Jaji Ngwala ambaye alitumia takribani
saa 1:15 kusoma huku hiyo alisema katika utoaji wa hukumu hiyo haukuzingatia
vipengele muhimu vya kisheria viilivyotumika na mahakama ya wilaya kumtia
hatiani Mchungaji Mwasumbi.
“katika rufaa hii ni kweli kuna mambo
mengi ambayo yanaonekana kukiukwa katika utoaji wa hukumu, kama zilizovyoweza
kuanishwa na wakili wa utetezi hivyo na mimi nakubaliana na wakili Mwakagamba
(wakili wa utetezi) kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa kisheria kwenye hukumu
hiyo” alisema
Aliongeza kwamba kama ilivyoelezwa na
wakili Mwakagamba, muda wa lilitopotekea tukio hilo na liliporitiwa
kwenye vyombo vya usalama unaonekana kuchelewa na kukinzana, lakini pia
ushahidi ulitolewa mahakamani hapo na Mhanga ulionekana kujichanganya
hivyo haujaonesha mrufani kutenda kosa hilo’.
Awali Jaji Ngwala alimwita mchungaji
Mwasumbi kuwa ni mende, na ni mtu hatari sana katika jamii kwa kosa kama hilo
na hafai kuwa katika jamii jambo lililowafanya watu waliokuwa wakifuatilia
mwenendo wa hukumu hiyo kuanza kuinamisha vichwa chini akiwemo Katibu wa Kanisa
la Uinjisti Bwana Mwakasole.
Lakini baadaye, Jaji Ngwala
alionesha hisia zake kwamba kutokana na kujichanganya kwa ushihidi hususani wa
shahidi namba moja ambaye ni binti aliyefanyiwa kitendo hicho hivyo kumtoa
hivyo na haonekani kama ana kosa.
Alisema ‘Nasema hivi mtu huyu alikuwa
ni mende na ni hatari sana katika jamii asiyefaa kwa namna yoyote ile na
anastahili adhabu kali laiti kama ingethibitika hivyo, lakini hapa ushahidi
umeshindwa kuthibitisha hili hivyo ana haki ya kuachiwa huru’.
Hata hivyo, Jaji Ngwala alisema kuwa
kwa upande wa Jamhuri ambao ulikuwa ukiongozwa na wakili wa Serikali, Prosister
Paul una haki zote za kukata rufaa na kesi kuanza upya endapo utaona
haujaridhika na hukumu hiyo.
Wakili aliyekuwa akimtetea Mchungaji
Mwasumbi alisema kuwa katika rufaa ya mteja wake aliwasilisha sababu saba za
kupinga hukumu hiyo ambapo alidai kuwa hakimu wakati wa kutoa hukumu hiyo
alikosea kisheria na haki muda wa kuripotiwa kwa shauri hilo kwa vyombo vya
usalama na lilipotokea ulikinzana na kwamba aliegemea kwa ushahidi wa Mhanga
tu.
Sababu zingine alidai kuwa hakimu
aliegemea katika ushahidi au vidhibiti ambavyo awali alivikata mwenyewe,
pia alidai kuwa hakimu hakuangalia uhalisia kosa lenyewe na badala yake
alionekana kutoa maoni yake binafsi.
Lakini sababu nyingine wakili
Mwakagamba alisema kuwa hakimu huyo, aliegemea ushahidi ambao ulijichanganya,
wendesha mashtaka walishindwa kuwapeleka mahakamani hapo mashahidi
wa msingi katika kesi hiyo, hakimu aliegemea upande wa vyeti vya watoto wawil
waliodaiwa ni wa Mchungaji Mwasumbi ambapo vyeti vilidurufiwa (photocopy) na si
vyeti halisi na mwisho hakimu huyo alitoa hukumu ambayo haikufuata
mtiririko uliosahihi wa mashahidi husika.
Akizungumza na Mbeyayetu blog, mtoto wa
Mchungaji Mwasumbi, Elizabeth Mwasumbi alisema anamshukuru Mola kwa
kumwezesha Jaji Ngwala kwa kutenda haki katika rufaa ya baba yake.
Alisema; ’Mimi na wenzangu tulikuwa na
wakati mgumu sana pindi baba yetu akiwa ndani, kwani mimi niliathirika sana
kiafya na kiuchumi nilishindwa kufanya shughuli yoyote kutokana na mawazo
lakini namshukumuru Mola kwa kutenda haki’.
Hata hivyo nje ya Mahakama ndugu na
jamaa waliofurika kusikiliza hatma ya Rufaa hiyo waliokuwa na hamu ya kumlaki
kwa furaha Mchungaji Mwasimbi ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili
kushindwa kutokana na Maafisa wa Magereza kumpeleka Gerza la Ruanda kukamilisha
taratibu za Magereza
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)

0 Responses to “MCHUNGAJI ALIYEFUNGWA MIAKA 30 JELA KWA UBAKAJI AFUTIWA HUKUMU, MAHAKAMA YAMUACHIA HURU ”
Post a Comment