Tuesday, June 17, 2014
TANZANIA YAPATA BILIONI 24.1 KUSAIDIA BAJETI YA SERIKALI.
Do you like this story?
Wakati
wizara ya fedha ikiendelea na majadiliano ya Bajeti ya Serikali mjini Dodoma,
Serikali ya Japan imetoa kiasi cha Yen za Kijapani bilioni 1.5 ambazo ni sawa
na shilingi bilioni 24.1 za kitanzania kutoka Serikali ya Japani kwa ajili ya
shughuli za maendeleo hapa nchini.
Akizungumza
katika hafla hiyo ya kutiliana saini , Waziri Mkuya aliishukuru Serikali ya
Japani kwa kuwa na ushirikiano mzuri na Tanzania.
“Mkopo huu utachangia bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2014/2015, na fedha hizo zitaelekezwa katika sekta ya Maji, Elimu na Afya” alisema Waziri Mkuya.
Aidha, Mkuya aliendelea kusema kuwa, “tunatoa shukurani kwa Serikali ya Japani kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiitoa ambayo imeleta mafanikio makubwa nchini ambapo hivi sasa tumeona umaskini unapungua na kipato kinaongezeka kwa wananchi kwa mujibu wa taarifa ya Sensa ya watu na makazi ya 2012”.
Akijibu swali kuhusu fedha hizo za mikopo kuchelewa kufika, Waziri Mkuya alisema kuwa changamoto kubwa ambayo Serikali imekuwa ikiipata ni kutokana na taratibu za sera za nchi husika ambapo kila nchi wana sera zao.

Kwa
upande wake Balozi wa Japan Nchini Tanzania Masaki Okada alisema kuwa msaada
huo unahusiana na ushirikiano wa pamoja na Benki ya Dunia katika mkopo wa kumi
na moja wa kusaidia kupunguza umaskini ambao umekuwa ukitolewa tangu mwaka
2001.
Mikopo
hiyo imekuwa ikitolewa kwa masharti ya mkataba wa mkopo nafuu wa riba ya
asilimia 0.01 kwa Serikali hapa nchini.
Balozi
Okada alisema kuwa nchi yake imekuwa ikitoa mikopo mabalimbali ili kusaidia
Serikali ya Tanzania katika kupunguza umaskini ambapo misaada hiyo imekuwa
ikitumika kufuatana na GBS hapa Tanzanaia kwa kutoa fedha moja kwa moja ambazo
zinalenga kuharakisha juhudi za kupunguza umasikini hususani MKUKUTA.
Naye
Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) nchini
Yasunori Onioshi alisema kuwa shirika lake litaendelea kushirikiana na
Serilkali ya Tanzania katika kusaidia bajeti yake kwani Tanzania inakua kwa
haraka na mahitaji yake yanaendelea kuongezeka kila mara.
Makampuni
ya Kijapani yanayofanya kazi na Serikali ya Tanzania ni pamoja na Kampuni ya
Sigara (TCC) inayomilikiwa na Kampuni ya Kimataifa ya Tumbaku ya Kijapani,
Panasonic Energy Tanzania na JICA.
Hali
ya hewa ya Dodoma ni baridi na majadiliano kuhusu Bajeti ya Serikali yameanza
na yanaendelea.
Imetolewa na:
Msemaji Mkuu
Wizara ya Fedha
16/06/2014
Imetolewa na:
Msemaji Mkuu
Wizara ya Fedha
16/06/2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TANZANIA YAPATA BILIONI 24.1 KUSAIDIA BAJETI YA SERIKALI.”
Post a Comment