Tuesday, June 17, 2014
WANAOVAA VIMINI, MAVAZI YANAYOBANA NA KUACHA MAUNGO WAZI YAPIGWA MARUFUKU MAHAKAMA YA KINONDONI
Do you like this story?
IMEBAINIKA
kuwa miongoni mwa wale wanawake 20 waliodai kufanyishwa ngono na waganga wa
kienyeji ‘sangoma’ ili kupata ujauzito baada ya kukaa muda
mrefu bila watoto, wamo wake wa vigogo Bongo, Uwazi limechimba.
Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu kwa baadhi ya wanawake hao umebaini kuwa, waume wao wanafanya kazi katika nyadhifa za juu serikalini, wengine ni wastaafu na kwamba waume hao hawajui kinachoendelea.
Kwa mujibu wa mwanamke mmoja (jina lipo), katika sakata hilo kuna wake wa maprofesa, kanali mstaafu wa JWTZ na mmoja ambaye mume wake aliwahi kuwa kamanda wa polisi wa mkoa (RPC) ambaye kwa sasa naye ni mstaafu.
Mwanamke huyo alizidi kudai kuwa, ndoa moja katika hizo ilivunjika baada ya mume kubaini kuwa, mkewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa sangoma hao.
Uchuguzi zaidi ulibaini kuwa zaidi ya nguo za ndani ‘kufuli’ za wanawake zaidi ya 20 zilizokutwa na polisi kwa sangoma hao maeneo ya Tandika jijini Dar es Salaam zilikuwa zimeshavaliwa hivyo hakukuwa na mpya jambo lilionesha kuwa, zilivuliwa wakati wa tukio linalodaiwa lilikuwa na kutengezea dawa. “Sisi tuliamua kutoa taarifa polisi kwa sababu tumekuwa tukifanya ngono na wale waganga kwa muda mrefu bila kupata ujauzito na mbaya zaidi tulishatumia mamilioni ya pesa baada ya kuuza mali zetu, zikiwemo nyumba,” alisema mwanamke huyo nje ya kituo cha polisi.
Wanawake hao ambao hawakupenda majina yao yatajwe kwa kuhofia waume zao kujua, walisema ni kweli baadhi yao wamekaa katika ndoa kati ya miaka nane hadi 10 bila kupata watoto wala mimba Hata hivyo, baadhi yao walirudishiwa fedha zao baada ya Kamanda Kiondo kuwabana waganga hao.
Wiki iliyopita Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke chini ya Kamanda, SACP Englibert Kiondo liliwatia nguvuni sangoma wawili wakiwa na matunguli na zana nyingine za kuagulia binadamu Vitu hivyo viliteketezwa moto kwenye Kituo cha Polisi Temeke mbele ya waandishi wa habari.
“Ninaamini kuwa kwa vitendo hivyo vya kujamiiana ni hatari na huu ni ubakaji, kwani kuna uwezekano wa kuambukizana maradhi mbalimbali ikiwemo Ukimwi, kwa hiyo hizi zana nazichoma moto,” alisema Kamanda Kion Waliokamatwa katika zoezi hilo ni Juma Mohamed (32) na Abdallah Musa (25) ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo.do.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAOVAA VIMINI, MAVAZI YANAYOBANA NA KUACHA MAUNGO WAZI YAPIGWA MARUFUKU MAHAKAMA YA KINONDONI ”
Post a Comment