Thursday, June 19, 2014

TRA MBEYA YAINGIA NA HOFU.



MBEYA. Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoani mbeya  imeingiwa na hofu kutokana na uchumi  wa mkoa huo kuporomoka.

Inasema hali hiyo inachangiwa na wafanya biashara  mkoani humu kuingiza pombe haramu za viroba  na vipodozi vilivyopigwa marufuku  kwa matumizi ya binadamu kutoka nchi jirani ambyo havilipiwi kodi.

Meneja wa TRA mkoani  hapa anord maimu alitoa kauli hiyo juzi wakati wa kazi utekelezaji wa shehena  ya vipodozi  vyenye  viambata  vya sumu pombe haramu na vyakula vilivyokwisha muda wake vinavyofikia takribani  sh 40 milini.

Alisema kutokana na kasi ya uingizwaji  wa bidhaa hizo itafika mahala viwanda mkoani humo vitaacha  kuzalisha bidhaa  hizo na hat wenye viwanjd nje ya mkoa huo watasitisha kupeleka bidhaa zao  kutokana  na kukosa soko.

Bidhaa hizi zinaingizwa kwa njia ya panya licha ya kupigwa marufuku sisi haturuhusiwi kuzitoza kodi ya aina yoyote alisema maimu

0 Responses to “TRA MBEYA YAINGIA NA HOFU.”

Post a Comment

More to Read