Friday, June 20, 2014

WABUNGE WAHOJI KUTOFAUTIANA KWA TAARIFA ZA MAPATO YA SEKTA YA MADINI.



Baadhi ya wabunge wamelalamikia kutofautiana kwa taarifa za mapato husani katika sekta ya madini  na kutaka  kamati ya madini kukaa pamoja na kamati ya viwanda na biashara kupitia mikataba yote ya madini na kuishauri serikali kuvunja mikatapa itakayoonekana haina maslahi kwa taifa.

Wakichangia mjadala wa mwelekeo wa  mpango wa maendeleo  pamoja na bajeti ya mwaka 2014/25, baadhi ya wabunge bila ya kujali itikadi za vyama vyao wamelalamikia takwimu  za mapato katika sekta ya madini kutokuwa za kweli.

Katika mkutano huo wa kumi na tano kikao cha thelathimni na sita wamesema kitendo vya wizara mablimbali  kutofuata  sheria  na kukosekana kwa miiko ya uongozi kumechangia ongezeko la rushwa na ufisadi  na kuwa janga kubwa  katika taifa na kushangazwa na taarifa za mapango wa maendeleo wa taifa kutogusia tatizo la rushwa jambo linaloweza kusababisha mpango huo kutotekelezeka

0 Responses to “WABUNGE WAHOJI KUTOFAUTIANA KWA TAARIFA ZA MAPATO YA SEKTA YA MADINI.”

Post a Comment

More to Read