Friday, June 20, 2014

MAJENEZA SASA KUTOZWA KODI YA VAT.


Bungeni Dodoma

Majeneza

katika mkakati wake wa kuhakikisha inakusanya kodi ipasavyo  serikali imependekeza kutoza kodi ya  ongezeko  la thamani(VAT) katika maeneo  mbalimbali ikiwamo  uuzaji wa majeneza.

Katika miaka ya karibuni biashara ya majeneza Imekuwa kwa kasi kubwa hasa dar es salaam . pendekezo hilo limo katika muswada wa sheria  ya VAT unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni kuanzia june 27 mwaka huu  ambao pia umependekeza kutoa  kaodi hiyo katika maeneo mengine  ya usindikaji maziwa makandarasi  wazawa na sekta ya utalii.

Naibu waziri wa fedha  mwigulu nchemba alisema jana kuwa ngoja tusikilize wadau wanasemaje  lakini  lengo  la serikali ni kukuza uchumi na kukusanya mapato.

Alisema kuondoa misamaha ya kodi si njia pekee ya kuvutia uwekezaji na kusisitza   kuwa nchi nzima lazima ipate  fedha ili kupeleka huduma kwa wnanchi juzi taasisi ya sekta binafsi Tanzania TPSF ilikutana  na kamati ya bunge ya bajeti weizara ya fedha pamoja  na maofisa  wa mamlaka  ya mpato Tanzania TRA   kujadili  muswada huo na kutoa maoni yao huku  wabunge wengi wakiupinga  na kutaka uboreshwe.

Baadahi ya wdau wa sekta binafsi walimweleza  mwenyekiti wa kamti ya bajeti Andrew change  kuwa licha  ya muswada huo kutakiwa kufanyiwa marekebisha hata wao hawakushirikishwa ipasavyo  kwa malezo kuwa waliuona  novemba  mwaka  jana na kupewa wiki moja tu  ya kujadili na ktuoa maoni  yao.

Kwa masharti ya kutotajwa majina baadhi ya wajumbe  wa kamati ya bajeti walisema ni jambo la ajabu kwa serikali kuanza kukusanya kodi hadi katika uuzaji wa majeneza.

0 Responses to “MAJENEZA SASA KUTOZWA KODI YA VAT.”

Post a Comment

More to Read