Monday, June 9, 2014

WABUNGE WAUMBUANA KUPOKEA RUSHWA BUNGENI.


Mbunge wa Tunduru, Mtutura Mtutura (CCM).
Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Kiwanga (Chadema), amewaumbua wabunge wenzake kuwa wanapeana na kuchukua rushwa ndani ya Bunge.

Suzan aliyasema hayo juzi jioni wakati akichangia katika mkutano wa Chama cha Wabunge walio katika Mapambano dhidi ya Rushwa (APNAC). Suzan alisema vitendo hivyo vya rushwa vilionekana wakati wabunge hao walipokuwa wakiwachagua wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

“Rushwa ilikuwa ni wazi wazi ukienda chooni unapewa laki mbili (Sh200,000) unaondoka,”alisema Suzan.
Alisema wao kama viongozi ambao wanatunga sheria na wanatakiwa kuisimamia serikali wanapaswa kuwa waadilifu. Hata hivyo, Mbunge wa Njombe Kaskazini, Deo Sanga (CCM), alisema hakuna ukweli kuhusu jambo hilo la baadhi ya wabunge kuchukua rushwa hadi chooni.

Hata hivyo, Mbunge wa Tunduru, Mtutura Mtutura (CCM), alimuunga mkono Suzan na kusema suala hilo ni la kweli na kwamba kama Sanga hakuliona walikuwa wanamkimbia.

           

0 Responses to “WABUNGE WAUMBUANA KUPOKEA RUSHWA BUNGENI.”

Post a Comment

More to Read