Monday, June 16, 2014
WATU WAPATAO 48 WAUAWA KATIKA MASHAMBULIO KENYA.
Do you like this story?
Watu
wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kiislamu wameshambulia kituo cha polisi na
mahoteli na vijiji mjini Mpeketoni, pwani ya Kenya .
Makabiliano
makali yameripotiwa sehemu kubwa ya Jumapili usiku huku wakaazi wakitorokea
maeneo ya msitu karibu na kisiwa cha Lamu..
Shirika
la msalaba mwekundu linasema kuwa hadi kufikia sasa watu 48 wanahofiwa kuuawa kartika
shambulizi hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo.
Hata
hivyo vyombo vya habari vinasema idadi hiyo huenda ikawa juu zaidi.
Shambulizi
lilifanyika usiku wa kuamkia leo watu waliokuwa wamejifunika nyuso zao wakiwa
wamejihami vikali walivamia vituop vya polisi , hoteli na benki.
Shambulizi
hilo linakuja siku kadhaa baada ya serikali ya Uingereza kufunga ofisi zake kwa
hofu ya usalama.
Duru
za jeshi la Kenya zimearifu kuwa wapiganaji hao hawajajitambulisha ni wa kundi
gani.
Baadhi
ya walioshuhudia wamearifu kuwa wameona maiti kadhaa na majeruhi wengi japo
Polisi hawajathibitisha ni watu wangapi wameuawa.
Kenya
imekumbwa na mashambulio kadhaa kutoka kwa wapiganaji wa kisomali wa Al Shabaab
tangu ipeleke wanajeshi wake ndani ya Somalia mwaka wa 2011.
Duru
kutoka kisiwa cha Lamu zimearifu kuwa wapiganaji hao walifika katika malori
mawili na kurusha kifaa kama bomu ndani ya kituo cha polisi kisha wakavamia na
kuiba silaha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WATU WAPATAO 48 WAUAWA KATIKA MASHAMBULIO KENYA.”
Post a Comment