Monday, June 16, 2014

WAMBURA KUENGULIWA TENA SIMBA.



Kamati ya Uchaguzi ya Simba imemuondoa kabisa Michael Wambura katika mchakato wa uchaguzi wa Simba kwa madai kuwa amevunja taratibu za uchaguzi.

Akiongea na waandishi mchana katika ukumbi wa Serengeti, JB Belmonte Hotel jijini Dar, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Simba Dr. Damas Ndumbaro amesema Wambura amerudia kosa kwa kufanya kampeni kabla ya wakati kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi.

Kamati hiyo imeeleza kuwa TFF haina mamlaka kikatiba kusimamisha uchaguzi wa Simba kwa hiyo uchaguzi huo utaendelea kama ulivyopangwa kufanyika June 29 mwaka huu.

0 Responses to “WAMBURA KUENGULIWA TENA SIMBA.”

Post a Comment

More to Read