Monday, July 14, 2014
ASHAURI OFISI ZA SERIKALI ZOTE KUHAMIA DODOMA ILI KUPUNGUZA MSONGAMANO.
Do you like this story?
Serikali imeshauriiwa kuendeleza mchakato wa kuhamishia ofisi
zote zake mkoani Dodoma kwenye makao makuu ya nchi yetu ili
kuweza kupunguza msongamano wa watu na magari.
Hayo yalisemwa na Mtanzania Mzalendo, John Lyasenga wakati akizungumza na
waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano Idara ya Habari (MAELEZO)
jijini Dar es Salaam.
“ Kutokana na jiji la Dar es Salaam kuwa na msongamano wa watu na
foleni za magari, kuna umuhimu kwa Serikali kufikiria suala hili la kuhamishia
ofisi zake na huduma zingine muhimu kwa mji huo mkuu wa Tanzania kwa ni kwa
kufanya hivyo kutaleta fursa kwa wakazi wa mji huo,”alisema
Lyasenga.
Aidha aliongeza kuwa faida za kuhamia Dodoma ni pamoja na
kuwepo kwa fursa mbalimbali kama vile ajira ,kuongeza pato la mkoa kupitia
ujenzi wa viwanda vitakavyoongeza uzalishaji na kupunguza maafa kwa jiji
la Dar es Salaam kama vile mafuriko kutokana na wingi wa watu.
Mkoa wa Dodoma ina ukubwa wa eneo 41,000 kilomita za mraba na idadi ya
watu ni 2,083,588 kutokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ASHAURI OFISI ZA SERIKALI ZOTE KUHAMIA DODOMA ILI KUPUNGUZA MSONGAMANO.”
Post a Comment