Monday, July 14, 2014

JESHI LA POLISI ZANZIBAR LIMEMTIA MBARONI MMOJA WA WATUHUMIWA WA TINDIKALI.



 Makachero wa Jeshi la Polisi Zanzibar, wamefanikiwa kumtia mbaroni mmoja wa washukiwa wa matukio ya tindikali visiwani hapa Alawi Mohammed Silima (25) mkazi wa Fuoni Melinne nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema mtuhumiwa anahusishwa na tukio la kumwagia tindikali Sheha wa Shehia ya Tomondo mjini Zanzibar Bw. Mohammed Omar Saiidi Kidevu kabla ya kutoweka.

Inspekta Mhina amesema, Mtuhumiwa huyo ambaye kwa muda mrefu alikuwa akisakwa na Polisi kwa kuhusina na tukio hilo, alikamatwa juzi usiku akiwa mafichoni katika enero Fuoni baada ya taarifa za kiintelijensia kubaini kuwepo kwake.
 
Bado Makachero hao wanaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo kwa lengo la kuubaini mtandao mzima wa matukio mbalimbali yakiwemo ya tindikali yaliyotokea siku za nyuma visiwani humo.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kunatokana na taarifa za siri za raia wema ambapo Jeshi la Polisi lilikua likiendelea na upelelezi wa chini kwa chini wa kumbaini mtuhumiwa na mahali alipojificha.
 
Baadhi ya wananchi wa Zanzibar wamepongeza kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kuliomba Jeshi la Polisi kuendelea na juhudi zake za kuwafsaka watuhumiwa wengine wanaohusika katika matukio menginne kama hayo siku za nyuma viisiwani hapa.
 
Tukio la kumwagiwa tindikali kwa Sheha huyo, lilitokea majira ya saa 2.45 usiku Mei 22, mwaka jana, wakati Sheha huyo alipokuwa akirudi nyumba akitoka kuchota maji nyumba jirani. na kujeruhiwa vibaya mgongoni, kifuani, sikio na jicho la upande wa kulia.

0 Responses to “JESHI LA POLISI ZANZIBAR LIMEMTIA MBARONI MMOJA WA WATUHUMIWA WA TINDIKALI.”

Post a Comment

More to Read