Wednesday, July 23, 2014

MANISPAA ZA JIJINI DAR-ES-SALAAM ZAJIIMARISHA KATIKA UKUSANYAJI WA KODI ZA MAJENGO.


Waziri wa fedha, mhe. Saada Mkuya


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mwandisi Mussa Natty alisema kuwa Halmashauri yake ina wenyeviti wa mitaa wapatao 171na watendaji wa kata 34 ambao wanashiriki katika kufanya kazi ya kuainisha na kuorodhesha majengo kwa uthamini.

“Tumeweza kuyafanyia uthamini majengo 6,243 yenye thamani ya shilingi 1,493,360 na kodi inayotakiwa kukusanywa ni shilingi 2,538,712”. Alisema Mhandisi Natty.

Mhandisi. Natty ameongeza kuwa katika Manispaa yao wamefanya manunuzi ya vifaa vya ofisini ikiwemo magari kumi ili kurahisisha ufuatiliaji wa  mapato pia Halmashauri ya Kinondoni imefanikiwa kuanzisha mfumo wa malipo ya kielektroniki wa Maximalipo ambao umerahisisha malipo ya kodi katika maeneo ya karibu zaidi,kuondoa na kupunguza msongamano wakati wa malipo,kupata kumbukumbu za mlipa kodi kwa urahisi zaidi,uwazi na urahisi wa kufuatilia mapungufu.

Kwa upande wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyoBw. Photidas Kagimbo alisema kuwa wao wametoa mafunzo kuhusiana na uthamini kwa mkupuo kwa maafisa watendaji wa kata 30 na wenyeviti, pamoja na watendaji wa mitaa 180 wa Manispaa hiyo.

“Tumebaini jumla ya majengo 3,860 yenye thamani ya shilingi 145,652,498 na kiasi cha kodi ni shilingi 218,478. Alisema Bw. Kagimbo.

Aidha,Bw. Kagimbo amefafanua kuwa wamefanikiwa kuwapa watumishi uelewa wa matumizi ya TEHAMA katika utozaji wa kodi za majengo pia halmashauri imeagiza GPS Camera 5 zitakazozosaidia kuainisha ramani za majengo katika wilaya ya Temeke.

Kwa Halmashauri ya Ilala, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyoBw. Stima Kabikile naye alisema kuwa Kitengo cha uthamini cha Halmashauri yake kwa kushirikiana na viongozi wa kata na mitaa wameweza kubaini majengo 6,820 yenye thamani ya shilingi 989,640 na tozo ya shilingi 1,484,460.

“Pesa hizi zitokanazo na kodi za majengo zimesaidia kwa kiasi kikubwa katika suala la maendeleo ya halmashauri za jiji la Dar es Salaam kwasababu zinakusanywa na halmashauri husika”. Alisema Bw. Kabikile.

Bw. Kabikile ameongeza kwa kufafanua kuwa, baadhi ya matumizi ya pesa hiyo katika maendeleo ya manispaa yakeyametumika katikaununuzi wa magari,utengaji wa ofisi na samani zake zote,ununuzi wa vitendea kazi zikiwemo kompyuta, mashine ya kudurufu na vifaa vingine vya ofisi.

Halmashauri zimeweza kujitegemea kikamilifu katika ununuzi na utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kiserikali.
Ushirikishwaji wa wenyeviti wa mitaa na kata umepelekea majengo mengi kuainishwa kirahisi lakini bado kuna changamoto zinazozikabili Halmashauri hizi kama ukosefu wa vifaa vya kisasa na muhimu,kusambaa kwa majengo na mpangilio mbovu wa majengo.

Wananchi wanahimizwa kuona umuhimu wa kulipa kodi ili kukuza maendeleo ya wilaya zao na pia wanaaswa kuepuka kufichana majina ya wamiliki halali wa majengo pindi wathamini wanapofika katika majengo yao kwasababu moja ya changamoto kubwa ambayo wathamini wamekuwa wakikukbana nayo ni hiyo ambayo inawawia vigumu wathamini kufanya kazi yao.

0 Responses to “MANISPAA ZA JIJINI DAR-ES-SALAAM ZAJIIMARISHA KATIKA UKUSANYAJI WA KODI ZA MAJENGO.”

Post a Comment

More to Read