Monday, July 14, 2014

WAFANYAKAZI 20 WALIORUDI KINYEMELA TRL, WATAKIWA KUONDOKA HARAKA.


Amani Kisamfu ni Mkurugenzi wa TRL, katikati ni Naibu Waziri wa Uchukuzi Charles Tizeba akianika malalamiko ya wafanyakazi kulia ni Judith Ndaba, Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali watu kutoka Wizara ya Uchukuz


Zaidi ya wafanyakazi 20 wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) ambao walipunguzwa kazi mwaka 2007 na kulipwa stahiki zao kwa mujibu wa sheria, baadae wakarudi kwa mgongo wa nyuma na kufanya kazi tena mpaka leo, wanatakiwa kuondoka mara moja katika shirika hilo.


Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi Charles Tizeba katika mkutano na wafanyakazi wa shirika hilo, kujua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo wafanyakazi hao.

Bwana Tizeba alisema kuwa wafanyakazi hao walirudi kwa mgongo wa nyuma na kuanza kufanya kazi wakati walishapunguzwa hawatakiwi kuendelea kufanya kazi katika shirika hilo, kwani wao ndio watakuwa chanzo kikubwa cha migogoro katika shirika hilo.
Aidha alisema kuwa mishahara itapanda na reli itakarabatiwa kuanzia Tabora hadi Dar es Salaam ili kurahisisha usafiri kwa abiria mbalimbali wanaotumia usafiri huo.

Shirika hilo kwa sasa linakabiliwa na uchakavu wa miundombinu ya reli, viti vya kwenye mabehewa vimechoka, mabehewa machakavu pamoja na vichwa vyake.

0 Responses to “WAFANYAKAZI 20 WALIORUDI KINYEMELA TRL, WATAKIWA KUONDOKA HARAKA.”

Post a Comment

More to Read