Friday, September 12, 2014
AIBU: WATU WANNE WA FAMILIA MOJA WAKAMATWA WAKILIMA SHAMBA WAKIWA UCHI
Do you like this story?
Jeshi la polisi Mkoani Simiyu linawashikilia
watu wanne wa familia
moja kwa tuhuma ya kukutwa wakilima uchi wa mnyama
shambani kwa kile
kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu
Venansi Kimario
alisema tukio hilo limetokea septemba 2 majira ya
saa 12 asubuhi
katika kijiji cha Bushikwamala kata ya Kalemela
wilayani Busega Mkoani
Simiyu
Kimario alisema kuwa watu hao walikamatwa na jeshi
la polisi alfajiri
huko Bushigwamhala wakiwa wanalima kwenye shamba lao
na walipohojiwa
walidai kuwa walielekezwa na babu yao kipindi cha
uhai wake kuwa
wakilima uchi watapata mavuno mengi.
Kamanda Kimario aliwataja waliokamatwa kuwa ni
Makoye Kagoje (42), na mke
wake Neema Kigwela (31) pamoja na watoto wao, mmoja
wa kiume (15) na
wa kike (12) majina yamehifadhiwa.
Aidha Kimario alisema watu hao pamoja na watoto wao
wanashikiliwa na
jeshi la polisi kwa kukutwa wakifanya vitendo vya
ushirikina.
Babu yao alishafariki mwaka jana na aliwaambia kuwa
wakilima wapo uchi
watapata mavuno mengi, hivyo waliamua kufanya hivyo
kutokana na wosia
wa babu yao
Alisema baada ya jeshi la polisi kupata taarifa
kutoka kwa raia wema
liliweza kufika katika eneo hilo na kuwakamata
watuhumiwa hao wakiwa
wanaendelea kulima bila nguo.
Hata hivyo Kimario amewataka watu wasijishirikishe
kwenye
vitendo vya ushirikina na siyo kwamba ukilima uchi
utapata mazao mengi
tofauti na kufuata kanuni za kilimo bora, viongozi
wa madhehebu ya
dini na viongozi wa serikali tuwaelimishe watu
waachane na imani za
kishikina .
Na Faustine Fabian-Simiyu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AIBU: WATU WANNE WA FAMILIA MOJA WAKAMATWA WAKILIMA SHAMBA WAKIWA UCHI ”
Post a Comment