Thursday, March 5, 2015
WANANCHI MBEYA WAZUA MAKUBWA BAAADA YA KUZIPIGA KUFULI OFISI ZA TENESCO
Do you like this story?
Wateja wakiwa kwenye foleni ndefu wakinunua umeme wa Luku Asubuhi ya leo. |
Wateja wakiwa kwenye foleni ndefu wakinunua umeme wa Luku Asubuhi ya leo. |
(Picha na Fahari News)
Wakazi wa jijini hapa jana walizua
tafrani baada ya kufunga ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)
kwa muda wakidai kupewa majibu kuhusu tatizo la upatikanaji wa umeme lililodumu
kwa zaidi ya siku tano.
Tukio hilo lilitokea jana saa 4:00
asubuhi baada ya wateja hao kusubiri majibu kutoka kwa wahusika, ambao awali
walitangaziwa kuwa huduma hiyo ingeanza kupatikana juzi, lakini mpaka jana
tatizo hilo lilikuwa likiendelea.
Wakazi hao waliwafungia wafanyakazi wa
Tanesco wa kitengo cha malipo, wakisema kuwa hawafanyi kazi yoyote na hivyo
hawatakiwi kutoka nje. Hali hiyo ilidumu hadi askari wa walipowasili na
kuwashauri waondoke.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
ofisini hapo, wateja hao walisema baada ya kukosekana kwa huduma ya luku kwa
siku tatu, jana kupitia simu zao za mkononi walipokea ujumbe uliowataarifu kuwa
huduma hiyo ingeanza kutolewa jana kwa mawakala na katika ofisi za Tanesco,
hata hivyo hali haikuwa hivyo.
Mkazi wa Mwanjelwa,
Dickson Mwangunga
alisema watendaji wa shirika hilo wanatoa taarifa zisizo sahihi na kusababisha
usumbufu.
“Ni vema
kama wangetoa taarifa sahihi, watu tumefika hapa kwa ajili ya kununua umeme,
lakini huduma hiyo haipo. Baadhi yao wanatuambia eti hali bado haijatengemaa,
wengine wanasema tusubiri na muda unazidi kwenda, sasa nani mkweli? ndiyo maana
tumeamua kuzifunga ofisi zao watupe jibu sahihi lini huduma hii itatengemaa,”:- Mwangunga.
Hata hivyo, sakata hilo liliokolewa na
mkuu wa upelelezi wa Wilaya ya Mbeya, Kitinkwi Mtatiro ambaye alifika katika
ofisi hizo na kuwaomba wateja hao warejee nyumbani hadi watakapopewa taarifa ya
kurejeshwa kwa huduma na uongozi wa Tanesco.
“Nawaomba
mfungue milango ya ofisi, waacheni wafanye kazi hili ni tatizo limetokea. Hata
wao hawapendi karaha hii itokee ni vema mkawa watulivu msipende kujichukulia
sheria mkononi. Jambo hili linaweza kuvuruga amani,” :- Mtatiro.
Akizungumzia hali hiyo, meneja wa
Tanesco wa Mbeya, Amos Maganga aliwaomba wananchi kuwa watulivu kwa kuwa tatizo
hilo ni la kitaifa na mara mitambo itakaporekebishwa watajulishwa kupitia simu
zao za mkononi.
Jijini Dar es Salaam, wananchi
waliendelea kulia na tatizo hilo lililodumu kwa siku tatu mfululizo.
Baadhi yao wamelalamikia hasara
wanayoipata kwa sababu ya kukosa umeme na kushindwa kufanya kazi za uzalishaji
zinazotegemea uwapo wa umeme.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANANCHI MBEYA WAZUA MAKUBWA BAAADA YA KUZIPIGA KUFULI OFISI ZA TENESCO”
Post a Comment