Thursday, March 5, 2015
WANANCHI WA KIJIJI CHA ISONGOLE NA NDAGA WAINGIA KATIKA MGOGORO WA ARDHI
Do you like this story?
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mbeya moja wakiangalia mahindi yaliyofyekwa na wananchi wa kijiji cha ndaga kwa madai ya kutengeneza barabara .Picha na Ezekiel Kamanga |
Baadhi ya wananchi wakiwa wameshika miche ya mahindi iliyofyekwa na wakazi wa ndaga kwa lengo la kutaka kupitisha barabara katika eneo hilo |
Diwani kata ya Isongole( katikati) Bw.Laurence Nyasa akiwa pamoja na wananchi wake akiangalia uharibifu mkubwa uliyofanywa na wananchi wa ndaga Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya. |
Wananchi wa kijiji cha Mbeya Moja wakiwa katika mkutnao wa hadhara ili kupata suluhisho juu ya uharibifu huo. |
Mwenyekiti wa kijiji akihutubia wananchi |
Mkutano ukiendelea |
Na Ezekiel Kamanga,Mbeya
Wananchi wa Kijiji cha Mbeya Moja Kata ya Isongole na Kata ya Ndaga wameingia
kwenye mgogoro mkubwa baada ya wananchi wa Ndaga kufyeka mahindi bila ridhaa ya
wananchi wa Isongole kwa madai ya kupata barabara ya kupitishia mazao kutoka
shambani.
Tukio hilo la aina yake limetokea Februari 26
mwaka huu baada ya mkazi mmoja wa Ndaga ambaye pia ni mwenyekiti wa kitongoji
kuamuru wananchi wake kufyeka mahindi umbali wa kilomita zaidi ya moja bila
kujali mahindi yamekomaa au la na baadhi ya wananchi kuondoka nayo.
Baada ya kupata taarifa za mahindi kufyekwa
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbeya 1 Chesco Japhary alikwenda na kushuhudia
uharibifu mkubwa uliofanywa na wananchi wa Ndaga Mwenyekiti alitoa taarifa kwa
Diwani wa Kata ya Isongole Lawrence Nyassa.
Diwani baada ya kukagua mashamba hayo
alimshauri Mwenyekiti kutoa taarifa Polisi Kituo cha Kiwira ambapo baada ya
kuona ukubwa wa tukio waliwaamuru Viongozi wa Isongole kwenda kutoa taarifa
kituo kikuu cha Rungwe ili watuhumiwa wakamatwe na kujibu tuhuma
zinazowakabili.
Hata hivyo mpaka sasa Jeshi la Polisi
halijamkamata kinara wa uharibifu kwa kile kinachodaiwa kuwa yeye hawezi
kukamatwa na mtu yeyote na kwamba hili si tukio la kwanza kulifanya katika
Vijiji jirani vinavyopakana na Vijiji vya Ndaga.
Hivi karibuni wananchi wa Ndaka walichoma
hifadhi ya msitu wa Isongole na kufanya uharibifu mkubwa hali iliyofanya
wananchi kufanya juhudi za ziada kuokoa msitu huo usiteketee kabisa.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Isongole
Lawrence Nyassa amewataka wananchi wake kuwa na subira badala ya kujichukulia
sheria mkononi na pia amekerwa na vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa
na wananchi wa Ndaga mara kwa mara na tukio hili ni la tatu katika utawala
wake.
Vitendo vingine ni pamoja uchomaji wa
msitu,kun'goa mazao hususani viazi kwa madai ya kuchimba mtaro wa maji na sasa
kufyekwa kwa mahindi.
Pamoja na uharibifu wote huo hakuna fidia
yoyote waliyopewa wananchi wa Isongole licha ya gharama kubwa ya mbolea na pembejeo
za kilimo walizotumia ikiwa ni pamoja na mbolea za ruzuku hivyo kukwamisha
juhudi za serikali za kuondokana na njaa na kukuza uchumi.
Mwenyekiti wa Kijiji alimwagiza Afisa ugani
Felisia Mbuna kukagua mashamba yote ili kubaini thamani halisi ya hasara
iliyopatikana ili kila hanga alipwe fidia yake.
Kutokana na adha hiyo Kijiji kilifanya
mkutano wa hadhara Machi 4 mwaka huu ili kupata mustakabali wa suala hili.
Jamiimoja blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WANANCHI WA KIJIJI CHA ISONGOLE NA NDAGA WAINGIA KATIKA MGOGORO WA ARDHI”
Post a Comment