Saturday, March 7, 2015
JESHI LA POLIS MKOA WA GEITA LIMEWAKAMATA WAGANGA WA KIENYEJI 32 WANAOPIGA RAMLI CHONGANISHI.
Do you like this story?
Jeshi
la polisi mkoa wa Geita limewakamata waganga wa kienyeji 32 wanaopiga
ramli chonganishi katika msako uliofanywa hivi karibuni ili kuhakikisha mauaji
ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi yanakomeshwa kabisa.
Akizunguza na waandishi wa habari baada
ya kufanya msako na kuwakamata waganga hao kamanda wa polisi mkoa wa Geita Sacp
Joseph Konyo amesema wakati sasa umefika wa kuhakikisha mauaji yanayotokana na
imani potofu za kishirikina yanakomeshwa na ili kuyakomesha watu wa kwanza
kudhibitiwa ni waganga wa kienyeji wanaofanya shughuli zao pasipo kuzingatia
sheria na taratibu zilizowekwa na nchi.
Kamanda Konyo amesema upo ushahidi wa
wazi unaonyesha mahusiano ya karibu ya mauaji haya ya vikongwe na watu wenye
ulemavu wa ngozi na waganga wa kienyeji kwani ndio wahusika wanaoagiza viungo
vya Albino na ndio hao wanaopiga ramli za uongo kuonyesha kuwa vikongwe hasa
wanawake ndio wachawi.
Kamanda Konyo amesema serikali haiwezi
kuvumilia waganga wa namna hii wanaoipotosha jamii hivyo msako huu utaendeshwa
katika mikoa yote Tanzania bara ili kubaki na jamii salama isiyokuwa na vitisho
vya mauaji ya kikatili kama haya.
Baadhi ya wananchi mkoa wa Geita
wameipongeza hatua ya serikali kuanza sasa kuwachukulia hatua watuhumiwa wote
wanaopatikana na tuhuma za mauaji yanayotokana na mila potofu na ushirikina.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JESHI LA POLIS MKOA WA GEITA LIMEWAKAMATA WAGANGA WA KIENYEJI 32 WANAOPIGA RAMLI CHONGANISHI.”
Post a Comment