Wednesday, September 3, 2014
AZAM FC YAINGIA MKATABA WA UDHIMINI NA NMB, YAKADIRIWA KULAMBA BILIONI 1
Do you like this story?
Mwenyekiti wa Azam fc, Said Muhammad Said (wa pili kulia) akipokea jezi mpya kutoka NMB |
Na Baraka Mpenja, Dar
es salaam
BENKI ya NMB imeingia
mkataba wa udhamini wa miaka miwili na mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara,
Azam fc, utaohusisha gharama za usafiri na baadhi ya nyingine za uendeshaji wa
timu.
Mwenyekiti wa Azam
fc, Said Muhammad Said amewaambia waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu
hiyo yaliyopo, Azam Complex, Mbande, Chamazi, nje ya jiji la Dar es salaam kuwa
mkataba huo utaanza utekelezaji mara moja.
“Tumeupokea kwa
furaha mkataba huu na tunapenda kuwashukuru NMB kwa kuungana nasi”. Alisema
Said.
Naye katibu mkuu wa
Azam fc, Nassor Iddrisa ‘Father’ alifafanua kuwa NMB watanufaika na mkataba huo
kwa kutangaza nembo yao katika jezi za Azam fc, mabasi ya Azam fc na kuweka
mabango katika uwanja wa Azam Complex.
Pia Azam watavaa jezi
zenye nembo ya NMB kuanzia mazoezini na katika mechi za ligi kuu na mashindano
ya kimataifa.
Kwa upande wake
mkurugenzi mkuu wa NMB, Mark Weissing amesema mafanikio ya Azam fc ndio chachu
ya kuingia ushirikiano na timu hiyo.
Azam fc inakuwa timu
ya pili kuingia mkataba na taasisi ya kifedha nchini ambapo timu ya kwanza ni
Simba ambayo iliingia mkataba na NMB mwaka 2004, lakini 2004 walitemana.
Pia NMB iliwahi
kuidhamini timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa stars kati ya mwaka 2007 na 2010
ikiwa chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo ambaye kwasasa ni kocha mkuu wa
Yanga sc.
Wakati wa utiaji
saini wa mkataba baina ya Azam fc na NMB, watu wengi walikuwa na hamu ya kujua
una thamani gani.
Hata hivyo viongozi
wa Azam fc waligoma kutaja thamani ya mkataba huo, lakini taarifa za uhakika
zinasema mkataba huo unakadiriwa kuwa na thamani ya shilingi za Kitanzania
Bilioni 1.
Imeelezwa kuwa kwa
kila mwaka Azam fc watanufaika na shilingi milioni 500 za Kitanzania kutoka
NMB.
Tangu imeanzishwa
mwaka 2004 ba kupanda ligi kuu 2008, Azam fc inapata mdhamini kwa mara ya
kwanza .
Azam fc inakuwa
miongoni mwa timu chache za Tanzania zinazonufaika na udhamini.
Simba na Yanga ndio
timu pekee zilizokuwa zinanufaika na udhamini, kwa miaka mingi, lakini siku za
karibuni Mbeya City walivuna milioni 360 kutoka kwa Binslum.
Udhamini ni moja ya
vyanzo vya mapato kwa klabu za mpira wa miguu, lakini imekuwa changamoto kwa
timu mbalimbali kufikia mafanikio ya kupata wadhamini.
Siku zote mdhamini
anawekeza sehemu anayoweza kunufaika, hivyo sio rahisi kuweka fedha kwenye timu
yenye kiwango kibovu.
Kilio cha kukosa
udhamini kwa timu za ligi kuu kinasikika kila kukicha, lakini zimeshindwa
kutegua mtego huo tofauti na Azam fc na Mbeya City.
Hakuna haja ya kulia
kwa kukosa udhamini, ukiucheza mpira kwa nafasi uliyopata na kufanikiwa kama
Mbeya City, Azam fc, Yanga, na Simba, mabilioni na mamilioni yatakuja yenyewe.
Mafanikio ya Azam fc
yamewafanya walambe mabilioni kutoka NMB, na timu nyingine zinatakiwa kujipanga
kwa kutafuta mafanikio uwanjani zaidi ya kulia kila wakati.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AZAM FC YAINGIA MKATABA WA UDHIMINI NA NMB, YAKADIRIWA KULAMBA BILIONI 1”
Post a Comment