Wednesday, September 3, 2014
MTANANGE WA NGAO YA JAMII BAINA YA YANGA NA AZAM FC WASOGEZWA MBELE
Do you like this story?
MECHI ya Ngao ya
Jamii kuashiria kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa
2013/2014 baina ya mabingwa Azam fc na makamu bingwa, Dar Young Africans sasa
utapigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam septemba 14 badala ya septemba 13
mwaka huu kama ilivyopanga.
Shirikisho la soka
Tanzania limeamua kuusogeza kwa siku moja mchezo huo uliotakiwa kupigwa
jumamosi na sasa kupigwa jumapili kwa lengo la kuwapa fursa mashabiki wengi
kuuona.
TFF imesema
jumapili ni siku tulivu kuliko jumamosi na mchezo wa mwaka huu utaambatana na
shughuli za kijamii ikiwemo uchangiaji wa damu.
Pia sehemu ya mapato
ya mchezo huo yatapelekwa katika shughuli ya kijamii iliyochaguliwa.
Mechi hiyo itapigwa
ikiwa ni wiki moja kabla ya kuanza kwa ligi kuu septemba 20 mwaka huu ambapo
Yanga wataanzia ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar katika dimba la Jamhuri mkoani
Morogoro.
Mnyama Simba atakuwa
uwanja wa Taifa siku moja baada ya kufunguliwa kwa ligi kuu (septemba 21 mwaka
huuu) dhidi ya Wagosi wa Kaya, Coastal Union.
Azam fc watakuwa
nyumbani Azam Conmplex kuchuana na Polisi Morogoro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MTANANGE WA NGAO YA JAMII BAINA YA YANGA NA AZAM FC WASOGEZWA MBELE”
Post a Comment