Monday, September 8, 2014
JESHI LA POLISI LAKAMATA BUNDUKI NA MABOMU TUKIO LA UJAMBAZI KITUO CHA POLISI.
Do you like this story?
Bunduki 7 na mabomu 10 yaliyokamatwa huko Bukombe |
Habari
zilizotufikia hivi punde ambazo bado siyo rasmi zinasema kuwa jeshi la polisi
mkoani Geita limekamata bunduki saba (pichani) na mabomu 10 eneo la
Ushirombo wilaya ya Bukombe.
Inasadikiwa kuwa bunduki hizo ni kati ya bunduki kumi zilizoporwa na majambazi yaliyovamia kituo cha polisi Bukombe na kufanya mauaji ya askari polisi wawili waliokuwa zamu usiku wa kuamkia jana na kujeruhi askari wawili.
Tunaarifiwa kuwa Bunduki zilizokamatwa nne ni SMG na tatu aina ya Shotgun pamoja na panga zimepatikana katika tanuru la kuchomea matofali zikiwa zimefichwa pamoja na mabomu hayo.
Habari zinasema kuwa katika msako huo mkali unaoendelea, Jeshi linaloendelea kufanya kazi nzuri limekamata watu watatu pia na mwalimu mmoja wa shule ya sekondari Ushirombo anayedaiwa kushiriki katika tukio la jana.
Tumearifiwa kuwa jeshi la polisi linaendelea kufanya msako mkali ili kuwakamata wahusika wote na silaha zote zilizoporwa na majambazi.
Tunasubiri jeshi la polisi kutoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JESHI LA POLISI LAKAMATA BUNDUKI NA MABOMU TUKIO LA UJAMBAZI KITUO CHA POLISI.”
Post a Comment