Friday, September 5, 2014

JIJI LA MBEYA KUPATIWA WATAALAM NA NHC.


Meya wa jiji la Mbeya Bw Athanas kapunga akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari Ofisini kwake

Meya wa jiji la Mbeya wakwanza kushoto akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NHC  Bw.Nehemia Mchechu walipotembelea eneo la Stendi kuu ya Mabasi jijini Mbeya  kwa lengo la kutazama eneo litakalo faa kwa ajili ya ujenzi mpya wa stendi hiyo utakaosimaiwa na NHC. -



Shirika la nyumba la Taifa NHC limekubali kutoa timu ya wataalam watakaosaidiana na Halmashauri ya jiji la Mbeya katika  suala zima  la uchoraji  mpya wa ramani (MasterPlan) itakayotumika kwa ajili ya ujenzi wa makazi mapya katika halmasahuri ya jiji la mbeya.

Kauli hiyo imetolewa na Meya wa jiji la Mbeya Ndugu Athanas Kapunga mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo na wajumbe wa shirika hilo uliotembelea katika maeneo mbalimbali ya miradi inayotalajiwa kutekelezwa na shirika hilo la NHC.

Kapunga amesema mara baada ya kukutana na ujumbe huo ambao umeongozwa na Mkurugenzi wa shirika hilo Ndugu Nehemia Mchechu umelidhia kupeleka timu hiyo ya wataalam ambayo inashirikiana moja kwa moja na wataalam wa halmashauri hiyo ya jiji la Mbeya katika kutengeneza mpango huo.

Aidha amesema timu hiyo itaingia jijini humo mapema mwezi Octoba mwaka huu ili  kuanza mkakati huo kwa kuanza na hatua ya utoaji wa semina kwa wataalamu hao wa jiji la mbeya hususani katika idara ya mipango miji.

Amesema maeneo ambayo yatapewa kipaumbele katika utekelezaji wa shughuli hiyo ni pamoja na eneo la Iwambi ambalo limegaiwa kwa wakazi wa jiji la Mbeya pamoja na eneo la stendi kuu ya mabasi jijini humo.
Hata hivyo Ndugu Athanas Kapunga ameweka wazi juu ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa soko jipya la kisasa katika eneo la Uhindini ambalo nalo ujenzi wake utakuwa chini ya shirika hilo la nyumba NHC.

0 Responses to “JIJI LA MBEYA KUPATIWA WATAALAM NA NHC.”

Post a Comment

More to Read