Friday, September 5, 2014

STARS YAIFUATA BURUNDI , 'ADEBAYOR', MORRIS, MANULA WATEMWA!




WANANDINGA 20 wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wanaondoka leo alfajiri kwenda mjini Bujumbura nchini Burundi tayari kwa mechi ya kimataifa ya Kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya nchi hiyo itayochezwa septemba 7 mwaka huu (jumapili).

Mholanzi, Mart Nooij, kocha mkuu wa Stars amewaambia waandishi wa habari kuwa amekiandaa vizuri kikosi chake na kina matarajiao makubwa ya kulipa kisasi cha kufungwa mabao 3-0 na Burundi Aprili 26 mwaka huu katika mechi maalumu ya kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.

Katika mechi hiyo iliyopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Stars iliyosheheni wachezaji waliotoka katika mpango maalumu wa maboresho ya Taifa Stars uliofanywa na shirikisho la soka Tanzania, TFF,  ilishindwa kuhimili makali ya washambuliaji wa Burundi kama vile Didier Kavumbagu na Amiss Tambwe.

“Natambua Burundi ina wachezaji wazuri kama Tambwe, Kwizera na Kavumbagu, lakini kwa kikosi tunachokwenda nacho tuna uhakika wa kufanya vizuri na kulipa kisasi kwani Burundi walitufunga nyumbani.” Alisema Nooij.
Nooij alisema kuwa wachezaji John Bocco, Aggrey Morris na Aishi Manula wameachwa katika msafara wa Taifa Stars kutokana  sababu mbalimbali.

Morris na Bocco ni majeruhi wakati Manula ameachwa kwasababu tayari Nooij ana makipa wawili, Mwadini Ali na Deogratius Munish ‘Dida’, hivyo hakuna sababu ya kwenda na kipa huyo kinda.

Nooij aliwataja wachezaji watakokweda Bujumburu kuwa ni makipa Mwadini Ali (Azam fc) na Deogratius Munishi ‘Dida’, (Yanga).
Wachezaji wengine ni Shomari Kapombe (Azam fc), Oscar Joshua (Yanga), Said Mourad (Azam fc), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Joram Mgeveke (Simba).

Wengine ni Saimon Msuva (Yanga), Erasto Nyoni (Azam fc), Himid Mao (Azam fc), Amri Kiemba (Simba), Haroun Chanongo (Simba), Salum Abubakary ‘Sure Boy’ (Azam fc), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Hamis Mcha ‘Vialli’ (Azam fc), Juma Luizio (Zesco United, Zambia), Mrisho Ngasa (Yanga), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu (wote TP Mazembe, DR Congo).
.

0 Responses to “STARS YAIFUATA BURUNDI , 'ADEBAYOR', MORRIS, MANULA WATEMWA!”

Post a Comment

More to Read