Tuesday, September 16, 2014
KIKONGWE AUAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA KISU CHA TUMBONI HADI UTUMBO KUTOKA NJE.
Do you like this story?
Mkazi wa Kijiji cha
Ilogi, wilayani Kahama, Ester Bundala (80), ameuawa kikatili kwa kuchomwa kisu
tumboni na kutolewa utumbo baada ya watu waliojifanya wagonjwa kwenda nyumbani
kwake kuomba msaada wa kuchemshiwa dawa.
Wauaji hao pia
walimchoma bibi huyo kisu sehemu ya moyo, mbavu na mkono wa kulia na kutokomea
kusikojulikana.
Mtoto wa bibi huyo,
Francis Paulo, akiongea kwa Uchungu alisema wauaji hao ambao walikuwa
wawili, walifika nyumbani kwao Ijumaa iliyopita saa 12 jioni wakilalamikia
kuumwa tumbo na kuomba msaada wa kuchemshiwa maji ili wachanganye na dawa waliyokuwa
nayo kujitibu.
Paulo alisema mama
yake aliwachemshia maji na kuwapa ili waweze kutengeneza dawa yao na baada ya
kunywa walipumzika wakisubiri wapate nafuu.
“Baadaye giza lilipoingia baba yangu
mzee Paulo Nshimbi (83) alikuja nyumbani kwangu kukamua maziwa kwa vile
sikuwepo na ndama walihitaji kupewa maziwa,” alisema
Paulo.
Anasimulia kuwa
kitendo cha mzee wake kuwaaga wageni kilitoa mwanya wa kumuua mama yake.
“Hata hivyo muda mfupi kabla hajakata
roho mzee alirejea na kumkuta mama anahangaika, utumbo ukiwa umetoka nje,
amepoteza damu nyingi na kumtajia jina...."fulani amenichoma kisu amekuja
kuniua”, alinukuu maneno aliyosema mama yake huku akitaja jina la muuaji (jina
linahifadhiwa).
Aliongeza kuwa muuaji
alitumia mbinu ya kukodi wageni hao alioshirikiana nao kumuangamiza mama yake
kwa vile alifahamu ratiba ya siku hiyo.
Paulo alisema siku ya
mauaji yeye na shemeji yake anayeishi na wazazi wake, alikwenda kijiji cha
jirani cha Bugarama kumsalimia mkwe wao aliyekuwa mgonjwa.
Alisema walitoa
taarifa kituo cha polisi Bugarama na watuhumiwa wandugu Andrea na Robert Mabala
wamekamatwa lakini mhusika ambaye ni mwanafamilia aliyetajwa na mama yao wakati
anakata roho hajaonekana.
Kaimu Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Shinyanya, Musa Athumani Taibu, alithibitisha kuwapo kwa
mauaji hayo na kueleza kuwa mtuhumiwa ametoroka na polisi inaendelea na msako.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KIKONGWE AUAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA KISU CHA TUMBONI HADI UTUMBO KUTOKA NJE.”
Post a Comment