Tuesday, September 16, 2014
SERIKALI YASEMA BUNGE MAALUM LA KATIBA LINA UHALALI KISHERIA NA KISIASA KUENDELEA.
Do you like this story?
Na Magreth
Kinabo,Dodoma
Serikali imesema
kwamba Bunge Maalum la Katiba linaendelea kwa mujibu wa Sheria, mjadala wa hoja
ya kusitishwa kwa Bunge hilo, umefungwa rasmi leo.
Aidha Serikali
imewaondoa hofu wananchi kwamba hakuna mgogoro wa kisiasa, hivyo waendelee na
shughuli zao za kujipatia kipato(riziki) kama kawaida, pia ipo macho kupitia
vyombo vyake vya usalama,itasimamia sheria na taratibu zilizowekwa ili
kuhakikisha taifa linaendelea kuwa na amani na utulivu.
Kauli hiyo imetolewa
leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha
Rose Migiro kwenye kikao cha Arobaini cha Bunge hilo wakati akitoa tamko
la Serikali kwenye mjadala wa mwisho wa kujadili sura zote 15 zilizobakia
za Rasimu ya Katiba Mpya.
“Bunge hili linaweza
kuendelea na shughuli zake. Nawaomba Watanzania wafahamu mjadala wa kusitisha
Bunge umehitimishwa hii leo kisheria na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,” alisema Dk. Migiro.
Dk. Migiro aliongeza
kuwa kwa taarifa walizonazo majadiliano baina na Mwenyekiti wa Kituo cha
Demokrasia Tanzania(TCD) pamoja na vyama vyote husika yataendelea Septemba 17
na 18, mwaka huu, kwa sababu mchakato huo si wa chama kimoja, wala viwili au
vitatu , bali mchakato wa Watanzania wote kupitia mfumo ambao umewekwa
wa vyama vyote kisheria.
Akizungumzia kuhusu
takwimu za wajumbe wa Bunge hilo, Dkt. Migiro alisema kuwa lina wajumbe
630, kati yao waliotoka nje ya Bunge hilo ni wajumbe 130 ni sawa na asilimia 21
ya wajumbe wote.
“Wajumbe waliobakia
ndani ya Bunge hili ni 500, sawa na asilimia 79 ya wajumbe wote, tukitazama
mambo ya takwimu kwa kutambua Kundi la 201. Imejitokeza dhana kwamba
wajumbe waliobakia humu ndani ni wa aina moja, hiyo si kweli,”alisema.
Dk. Migiro
alisema kati ya wajumbe 500, waliobaki katika Bunge hilo, 189, wanatoka
katika kundi la 201.
Alisema wajumbe
wengine waliobakia, 348 wanatoka upande wa Tanzania Bara, kati ya hao,
wajumbe 125 ni wajumbe wanaotoka Kundi la 201.
“ Tukiangalia upande
wa Zanzibar wajumbe waliobakia ni 152, kati yao wajumbe 64 wanatoka Kundi la
201.Tungependa kusisitiza Kundi la 201 ndio wajumbe ambao kwa wingi wao
kitakwimu na kimakundi wanawakilisha Taifa letu kwa sura zote.
“ Ni dhahiri
waliobakia humu ndani ni wengi, hii ina maana kwamba kwa kuzingatia matakwa ya
masuala ya kisheria kwa maridhiano, kwa majadialiano na kwa kushawishi hoja.
“Wajumbe
waliobakia ni wengi wana uhalali kisheria na kisiasa. Tutaendelea na
shughuli zetu kama sheria inavyotutaka, uwakilishi wa Bunge umetimia …
tuna wajibu wa kisheria wa kufanya yale tunayoyataka
kuyafanya,” alisisitiza huku akisema waliotoka nje kwa pande zote
mbili hawafikii theluthi moja.
Alifafanua kuwa vyama
vilivyotoka nje ya Bunge hilo, ni vitatu,vilivyobakia ndani ya ni 18
ambavyo vimesimamia na vinaendelea kusimamia umoja wa kitaifa wa nchi
yetu.
Akichangia mara baada
ya tamko hilo, mjumbe wa Bunge hilo, John Shibuda alimpongeza mtoa taarifa hiyo
ya Serikali na kuipongeza Serikali kwa kushinda kesi.
Aliwataka Watanzania
kuchuja kati ya siasa na maslahi binafsi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERIKALI YASEMA BUNGE MAALUM LA KATIBA LINA UHALALI KISHERIA NA KISIASA KUENDELEA.”
Post a Comment