Tuesday, September 16, 2014
MVUTA BANGI AUA WATU WATATU KWA KUWACHARANGA PANGA NA KUWACHOMA MKUKI HUKO GEITA
Do you like this story?
Matukio
ya mauaji ya watu wasio na hatia, yameendelea kuuandama Mkoa wa Geita, kufuatia
watu watatu kuuawa kwa kukatwa mapanga na kuchomwa mkuki huku mmoja akijeruhiwa
baada ya mtu mmoja anayesadikiwa ni mgonjwa wa akili kutekeleza unyama wake.
Tukio
hilo lililotokea jana asubuhi katika kijiji cha Nyamilyango wilayani Geita,
na aliyejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita ni
Mathayo Sindamsanga, na hali yake imeelezwa ni mbaya.
Mganga
Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Adam Sijaona, alithitibisha kupokea miili
mitatu iliyohifadhiwa hospitalini hapo pamoja na majeruhi mmoja.
Dk.
Sijaona aliwataja waliouawa kuwa ni Pindo Makono, Ndakazi Bertha Masabile na
Jacob Bukulu, ambao ni wakazi wa kijiji hicho.
Hata
hivyo, mtu huyo aliyesababisha mauaji hayo, alikamatwa na wananchi wenye hasira
na kisha kumfikisha kituo cha polisi.
Dk.
Sijaona alisema marehemu hao walifariki dunia kutokana na kuvuja damu nyingi
mwilini kufuatia muuaji kutumia panga na kuwacharanga na kisha mkuki kuwatoboa
miili.
Akizungumzia
tukio hilo, Diwani wa Kata ya Bugulula, Elisha Lupuga, alisema lililotokea juzi
saa 1:00 jioni katika kitongoji cha Misheni katika kijiji cha Nyamilyango baada
ya mtuhumiwa, Rashid Ramadhani, mkazi wa kijiji hicho kutumia mkuki na panga
kuwaua watu hao.
“Dhamira
yake mpaka sasa haijafahamika ilikuwa nini, lakini amekuwa na tabia ya kuvuta
bangi na kwa muda mrefu, hivyo tunahisi amevurugukiwa akili yake,” alisema
Lupuga.
Hata
hivyo, Lupuga alisema baadhi ya waliouawa walikuwa na mahusiano na mtuhumiwa,
lakini hakufafanua ni mahusiano ya namna gani waliyokuwa nayo.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Joseph Konyo, alithibitisha kutokea tukio hilo na
kwamba mtuhumiwa anashikiliwa katika kituo cha polisi akisubiri hatua za
kisheria kuchukuliwa dhidi yake.
Tukio
hilo limeibua upya simanzi na vilio kwa wananchi wa mkoa huo ambao mara kwa
mara wamekuwa wakikumbwa na matukio ya mauaji ya aina mbalimbali.
Hilo
ni tukio la pili ndani ya wiki moja baada ya usiku wa kuamkia Septemba 7, mwaka
huu, watoto wanne wa familia moja kuuawa kufuatia nyumba yao kuteketezwa na
moto katika kitongoji cha Elimu kata ya Kiangalala wilayani Geita.
Watoto
walioteketea na moto huo ni Reginald Robert (9) mwanafunzi wa darasa la nne na
Sofia (6) wa Shule ya Msingi Ukombozi na Remijius (4) wa chekechea pamoja na
Scolastika (15) aliyekuwa akisoma shule ya sekondari Mwatulole.
Katika
tukio hilo, baba wa familia, Robert Reginald (49), mkewe Angelina Reginald na
watoto Robert mwenye umri wa miaka miwili na miezi mitatu na Yohana (1),
walinusurika katika janga hilo.
NA RENATUS MASUGULIKO-geita
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MVUTA BANGI AUA WATU WATATU KWA KUWACHARANGA PANGA NA KUWACHOMA MKUKI HUKO GEITA”
Post a Comment